
Serikali
ya China kupitia Jeshi la Ukombozi la China, kikosi cha Anga limetoa
msaada wa ujenzi wa Chuo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Taifa kilichopo
Kunduchi, Dar es Salaam unaogharimu Shilingi Bilioni 56.
Ujenzi
huo wa awamu ya pili ya chuo hicho utakifanya kuwa cha kisasa na
miundombinu rafiki na kukiwezesha chuo hicho kudahili zaidi ya wanafunzi
100 kwa wakati mmoja baada ya ule wa awamu ya kwanza uliofanyika 2013
na kumalizika 2015.
Akizungumza
wakati wa kuweka jiwe la msingi Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga
Taifa, Dk Hussein Mwinyi, aliishukuru Serikali ya China kupitia jeshi la
ukombozi la watu wa China kwa msaada huo kwani utasaidia kuongeza kozi
na idadi kubwa ya wanafunzi.
Alisema
mafunzo yanatolewa katika chuo hicho yanalenga ulinzi wa taifa na
kimataifa kwa sasa na baadaye kiuchumi, kisiasa, kijeshi na kisayansi
katika mikakati ya maendeleo ya taifa.
Comments
Post a Comment