Waziri Biteko azitaka nchi za Maziwa Makuu Kudhibiti Raslimali Ardhi


Na Issa Mtuwa Dodoma
Nchi Wanachama wa Maziwa Makuu zimetakiwa kushikamana
kuunganisha nguvu katika kulinda na kusimamia matumizi ya raslimali
ardhi ikiwemo madini ili kunufaisha nchi hizo.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Madini Doto Biteko wakati akifungua
mkutano wa Kimataifa wa nchi Wanachama wa Maziwa Makuu
(International Conference on the Great Lakes Region - ICGLR)
unaofanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 11-12 Machi 2019 katika Hotel
ya Morena jijini Dodoma.
Biteko amezitaka nchi hizo kuunganisha nguvu ya pamoja katika kudhibiti
raslimali ardhi ikiwemo madini na kujiwekea utaratibu utakao dhibiti
shughuli za uzalishaji na biashara ya madini ili raslimali hizo zinufaishe
mataifa yao na zisitumike vibaya.
“Unganisheni nguvu kwa pamoja, wekeni utaratibu utakao wafanya nchi
wanachama kunufaika na raslimali ardhi/madini. Jitahidini kuhakikisha
raslimali hizo hazitumiki vibaya kama ilivyo kubaliwa kwenye itifaki, hivyo
lazima kuwe na utaratibu na sheria kwa kila nchi namna ya kudhibiti
uzalishaji na biashara ya madini,” amesema Biteko.
Naye, Mtaalam kutoka Wizara ya Madini, Mhandisi Assah Mwakilembe
amesema Mkutano huo unalenga kujadili na kupitia mfumo wa udhibitisho
wa mnyororo wa madini kwa lengo la kudhibiti uzalishaji na biashara ya
madini katika nchi za maziwa makuu kufuatia kuwepo tetesi zilizo kuwa
zinahusisha raslimali ardhi (Madini) na ufadhili wa vita katika nchi za
aaziwa makuu. (Region Certification Manual)
Akizungumza mara baada ya kuwasilisha mada kuhusu marekebisho ya
Sheria Madini ya Mwaka 2017 Mkurugenzi wa Idara ya Sheria kutoka
Wizara ya Madini, Edwin Igenge amesema kwa upande wa Tanzania,
imetekeleza itifaki ya pamoja ya nchi wanachama wa Maziwa Makuu kama
ilivyo kubaliwa.
Ameongeza kuwa, utekelezaji wa itifaki kwa Tanzania ni pamoja na
marekebisho ya sheria ya Madini ya Mwaka 2017 yaliyopelekea kuundwa
kwa Tume ya Madini ambapo shuguli zote za usimamizi wa raslimali
madini zimepewa Tume ya Madini ambapo kabla ya hapo shuguli hizo
zilikuwa chini ya Kamishna wa Madini.

Igenge amesema kuanzishwa kwa itifaki katika nchi za maziwa makuu
kulitokana na tetesi za uwepo wa matumizi mabaya ya raslimali ardhi
ikiwemo madini ambapo kipato cha raslimali hizo inasadikika kuwa zilikuwa
zinatumika kufadhili shuguli za za kivita katika nchi za maziwa makuu,
hivyo kupelekea kuanzishwa kwa itifaki ya pamoja kwa lengo la kudhibiti.
Mkutano huo wa kimataaifa unahudhuriwa na wajumbe kutoka Tanzania,
Burundi, Rwanda na wawakilishi wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani
(GIZ) na Sekretariati ya nchi wanachama wa Maziwa Makuu. Kwa upande
wa Tanzania inawakilishwa na Wizara ya Madini, Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Shirikisho la Wachimbaji Tanzania
(FEMATA), Chama cha Wanunuzi na Wauzaji wa Madini Tanzania
(TAMIDA), Tume ya Madini, Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Wakala
wa Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST).
Katika mkutano huo, Waziri Biteko aliambatana na Naibu Waziri wa Madini
Stanslaus Nyongo, Kamishna wa Madini Mhandisi Daivid Mulabwa,
Mkurugenzi wa Sheria kutoka Wizara ya Madini Edwin Igenge na baadhi ya
maafisa kutoka wizara ya Madini.

Comments