Washtakiwa wanne kati ya 12 wa kesi ya kusafirisha dhahabu Jijini Mwanza Wahukumiwa Baada Ya Kukiri Makosa

Washtakiwa wanne kati ya 12 wa kesi ya jinai namba 1/2019 ya kusafirisha shehena ya dhahabu kilo 323.6 na fedha taslimu Sh305 milioni wamekiri makosa yao.
Washtakiwa hao ni wafanyabiashara Hassan Sadiq, Emmanuel Mtemi, Kisabo Nkinda na Sajid Hassan..
Akitoa
hukumu baada ya washtakiwa kukiri makosa yao leo Machi 27, 2019, Hakimu
Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza, Rhodha
Ngimilanga aliwahukumu washtakiwa kwenda jela kati ya miaka mitano hadi
15 au kulipa faini kati ya Sh5milioni hadi Sh100 milioni.
Waliohukumiwa
adhabu hiyo ni wafanyabiashara Hassan Sadiq, Emmanuel Mtemi, Kisabo
Nkinda na Sajid Hassan waliokuwa wakitetewa na mawakili Emmanuel Safari
na Michael Nasimile.
Pamoja
na hukumu ya kifungo kwa muda tofauti na faini kulingana na makosa,
Mahakama pia imeamuru kutaifishwa kwa kilo 319 za dhahabu, fedha taslimu
Sh305 milioni, magari mawili, kilo sita za madini ya vito na mashine ya
kupima ubora wa madini.
Katika
hukumu yake, Hakimu Ngimilanga aliwatia hatiani washtakiwa katika
mashtaka sita ambapo kwa shtaka la kwanza washtakiwa wote wanne
wamehukumiwa faini Sh5 milioni au kifungo cha miaka 15 jela.
Katika
shtaka la tatu Mahakama imemtia hatiani mshtakiwa wa kwanza, Hassan
Sadiq na kumhukumu kulipa faini Sh5 milioni au kwenda jela miaka 15.
Washtakiwa
wote wanne pia wametiwa hatiani katika kosa la tano na kuhumiwa kulipa
faini Sh600, 000 kila mmoja au kifungo jela miaka mitano.
Mahakama pia imewahukumu washtakiwa kulipa faini ya Sh600,000 kila mmoja au kifungo cha miaka mitano jela.
Mshtakiwa
Hassan Sadiq pia ametiwa hatiani katika shtaka la nane na kuhukumiwa
adhabu ya faini Sh5 milioni au kwenda gerezani miaka mitano.
Katika shtaka la tisa, washtakiwa wote kila mmoja amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela au kulipa faini ya Sh5 milioni.
Wakati
wenzao wanne wakikiri makosa na kuhukumiwa, washtakiwa wengine wanane,
wote wakiwa ni waliokuwa askari polisi akiwemo aliyekuwa mkuu wa
operesheni mkoa wa Mwanza, Morice Okinda walikana mashataka na
kurejeshwa rumande hadi Aprili 10, kesi hiyo itakapoanza kusikilizwa
baada ya upelelezi kukamilika.
Wengine
wanaoendelea na kesi ni E. 6948 D/CPL. Kasala, F. 1331 PL. Matete, G.
6885 D/C Alex, G. 5080 D/C Maingu, G. 7244 D/C Timothy, G. 1876 D/C
Japhet na H. 4060 D/C David Kadama.
Comments
Post a Comment