WANANCHI WASHIKANA KUCHANGIA UJENZI WA SHULE















 Wananachi wa kijiji cha Mkange na Mtakuja kata ya Bugelenga
wilaya ya Bukombe mkoani Geita , wameshikamana kujichangisha kujenga
shule shikinzi  mbili kwenye vijiji vilivyoko mbali na shule ya msingi
Bugelenga kupunguza changamoto za wanafunzi  kutembea umbari mrefu
kutafuta Elimu hasa darasa la awali na lakwanza.

Ofisa mtendaji wa kijiji cha Mkange Matulanya Mabura alisema kunakaya
140 kila kaya sh 50,000 na wanafunzi wanalazimika kutembea umbali
mrefu wa kilomita 7 kwenda shule ya msingi Bugelenga wanapofika la
tatu au la Nne.
Mabura alisema wameazisha tena ujenzi  wa vyumba viwili Ofisi moja ya
utawala hadi usawa wa lenta nguvuza sh 5.5 milioni hadi kukamilika
yatagalimu sh 22.3 milioni.
Mbunge wa jimbo la Bukombe Doto Biteko akiwa naziara ya kwenda
anawashukuru wananchi na kuunga mkono nguvu za wananchi kwenye miradi
ya wananchi Machi 2 mwaka huu alichangia sh 3.6milioni kwa ajili ya
ukamilishaji wa madarasa mawili na ofisi ya walimu shule ya msingi
Mkange akiwa kijiji cha Mtakuja alitowa sh 2 milioni kuunga mkono
jitihada za wananchi.

Kaimu ofisa mtendaji wa kijiji cha Mtakuja Saguda Magadu alisema
kijiji kilianzisha mwaka 2012 vitongoji vitano na kuanza mikakati ya
maendeleo hadi 2016 walianza ujenzi wa shule ya msingi Baraka ambayo
inawanafunzi 170 na huwa wanalazimika kutembea umbari wa kilomita nne
kwenda shule mama ya Bugelenga wanapo fika daasa la tatu.

Magadu alisema katika ujenzi wa madarasa mawili yamejengwa na nguvu za
wananchi sh 4.6 milioni kwa kuchangishana sh 25,000 kati ya kaya 199
hadi kukamilika vyumba vya madarasa inaitajika sh 4.3 milioni
Biteko aliwaomba wananchi kuendelea kushirikiana katika miradi ya
maendeleo na kwamba shule hizi shikizi iwapo wananchi watachangia
kikamilifu na kkamilisha taratibu za kusajiliwa kisheria mwaka huu
itawapunguzia changamoto wanafunzi kutembea umbali mrefu.

Aliwaomba kuachana na siasa za kuwacheleweshea maendeleo badala yake
wazingatie kauli mbiu yake ya kusema na kutenda ili wawe wamoja waseme
watende hali ambayo italeta mabadiliko makubwa ya kimaendeleo hakuna
nchi iliyo pata maendeleo na kuwa na miradi mizuri sekta ya Elimu Afya
barabara bila wanachi kulipa kodi na kuchangishana wenyewe.

Ofisa Elimu taluma shule za msingi wilaya ya Bukombe Kassim  Musa
alisema wilaya inashule za serikali 78 nakwamba wananchi wahakikishe
wanashiamana kujenga miundombinu za shule ilizikizi vigezo vya
kusajiliwa ili serikali ilete walimu wa kutosha

Mkazi wa ijiji cha Mkunge Emmanuel Mayala alimushukuru mbunge kwa
kuwaunga mkono halimabayo inawapa hamasa ya kuendelea kuchangia
maendeleo.

Comments