TIMU ya soka ya Taifa, Taifa Stars, imekuwa miongoni mwa timu nne zilizofuzu kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) kutoka Ukanda wa Afrika Mashariki baada ya kuifunga Uganda 'The Crane' magoli matatu kwa sifuri.
Mechi
hiyo dhidi ya Taifa Stars na Uganda the Craines imechezwa katika Uwanja
wa Taifa jana (Jumapili, Machi 24, 2019) ambapo Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa aliwaongoza Watanzania kushuhudia mechi hiyo.
Taifa
Stars imefuzu michuano hiyo itakayofanyika mwaka huu nchini Misri baada
ya kupita miaka 39 tangu mara ya mwisho kucheza michuanohiyo.Timu hiyo
kwa sasa imeungana na Burundi, Kenya na Uganda kufuzu michuano hiyo.
Magoli
ya Simon Msuva, Erasto Nyoni na Agrey Morris yalichangia kuivusha
Taifa Stars, ambapoMsuva alianza kwa kuipatia gori timu ya Taifa ya
Tanzania dakika ya 20 baada ya mechi hiyo kuanza, Nyoni aliipatia Taifa
Stars goli la pili dakika ya 50 na dakika sita baadae Moris aliipatia
timu ya Taifa goli la tatu.
Kufuatia
ushindi huo wachezaji wote wa Timu ya Taifa ya Tanzania
wamejihakikishia kila mmoja kuondoka na kitita cha shilingi milioni 10
kutoka kwa Kamati ya Saidia Taifa Stars Ishinde inayoongozwa na Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Akizungumza
na wachezaji hao juzi wakati Waziri Mkuu alipotembelea kambi yao,
Makonda ambaye ndiye Mwenyekiti wa kamati hiyo alisema kamati yake
itatoa sh. milioni 10 kwa kila mchezaji wa timu hiyo iwapo timu itafuzu
kucheza michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON).
Kwa
upande wake, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangala yeye
aliwaahidi kuwapeleka katika mbuga yoyote ya wanyama watakayoichagua
kwa ajili ya mapumziko iwapo wachezaji hao wataibuka na ushindi katika
mechi dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
Comments
Post a Comment