Maelfu
ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wamejitokeza kwa wingi katika
viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kutoa salamu kwa Ruge Mutahaba
aliyegusa nyoyo za wengi ziliongozwa na Rais Dkt.John Magufuli, Rais
mstaafu wa awamu ya nne Dkt.Jakaya Kikwete aliyeambatana na mkewe pamoja
na Waziri mkuu Kassimu Majaliwa na mkewe Mary Majaliwa. Wakati huo huo
msanii Naseeb Abul maarufu kama Diamond Platnumz , Fleva Ali Kiba, Mwana
FA na Ommy Dimpoz pia waliwasili katika viwanja hivyo kwa ajili ya
kutoa salamu za mwisho.


Jeneza
lililobeba mwili wa marehemu Ruge Mutahaba ambaye aliyekuwa Mkurugenzi
wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Entertainment kwenye hafla
iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo
Jumamosi March 2, 2019 ( Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii) 

Msanii
wa muziki wa bongo Flava Nasibu Abdul "Diamond Platinumz" akiwasili
katika msiba wa marehemu Ruge Mutahaba ambaye aliyekuwa Mkurugenzi wa
Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Entertainment kwenye hafla iliyofanyika
katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumamosi March 2,
2019 

Msanii
wa muziki wa Bongo Fleva Ali Kiba pamoja na Mwana FA na Ommy Dimpoz
wakitoka kuaga mwili wa marehemu Ruge Mutahaba ambaye aliyekuwa
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Entertainment kwenye hafla
iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo
Jumamosi March 2, 2019. 

Msanii
wa muziki wa Bongo Fleva, Harmonize akiondoka mara baada ya kuaga mwili
wa marehemu Ruge Mutahaba ambaye aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na
Vipindi wa Clouds Entertainment kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja
vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumamosi March 2, 2019. 


Msanii wa kizazi kipya Barnaba akiondolewa ukumbini akiwa amebebwa baada ya kuishiwa nguvu kutokana na uchungu mkali alio nao.


Comments
Post a Comment