
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Katika
kukabiliana na changamoto ya Usafiri kwa maofisa elimu mikoa,Serikali
kupitia TAMISEMI imenunua takribani magari 26 kwa ajili ya Maofisa
elimu mikoa katika mikoa yote 26 Tanzania bara.
Hayo
yamesemwa Machi 27 jioni , jijini Dodoma na Waziri wa TAMISEMI
Seleman Jafo wakati akifunga mkutano mkuu wa 6 wa maafisa elimu
wilaya na mikoa Tanzania bara[REDEOA] ambapo amesema kuwa magari hayo
yatarahisisha usafiri kwa maafisa hao katika kutembelea shule mbalimbali
katika mikoa yao na kuibua changamoto na kuzifanyia ufumbuzi.
Mhe.Jafo
amesema huwa hapendi suala la uzembe katika ufuatiliaji hivyo
amemwagiza katibu mkuu wizara ya TAMISEMI ndani ya siku tisini magari
hayo yawe yameshapatikana na kukabidhiwa kwa maafisa elimu wa mikoa.
Waziri
Jafo amewataka Maafisa Elimu,Kujituma ,kujitoa na kuzipenda kazi zao
huku akiwataka kuwaheshimu na kuwahurumia watu wa chini yao wakiwamo
walimu na kuacha dhana ya kuwadharau na badala yake kuwatia moyo ili
wafundishe kwa kujituma.
Aidha
,Waziri Jafo amebainisha kuwa wizara yake hadi kufikia sasa
imeshatenga fedha zaidi ya Tsh.Bil.18 kwa ajili ya vifaa vya maabara
kwa shule 1200 hapa nchini.
Katika
hatua nyingine Waziri huyo wa TAMISEMI amezungumzia juu ya suala la
nidhamu ambapo amebainisha katika kizazi hiki kuna baadhi ya walimu
wamekuwa wakivaa mlegezo wakiwa wanafundisha .
Naye
Mwenyekiti wa Umoja wa Maafisa Elimu wilaya na mikoa Tanzania bara ,
[REDEOA] Bi.Germana Mung’aho ambaye ni afisa elimu kutoka mkoani Mtwara
amesema mambo yote waliyojadili watayachanganua huku akiwashukuru
wajumbe wote kwa kushiriki mkutano huo muhimu.
Mkutano mkuu wa Maafisa elimu wilaya na mikoa Tanzania
bara[REDEOA]Umekutanisha
maafisa elimu mikoa na wilaya kutoka mikoa yote 26 Tanzania bara na
kaulimbiu ya mwaka huu ilikuwa ni Elimu bora itatufikisha katika uchumi
wa kati ifikapo mwaka 2025.
Comments
Post a Comment