
Na Bakari Chijumba, Mtwara.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh.Dkt.John Pombe Magufuli,
anatarajia kufanya ziara ya kikazi mkoani Mtwara kuanzia 02 April hadi
April 04, Mwaka huu wa 2019 .
Akizungumza
na wanahabari leo Jumamosi 30 Machi 2019, mkuu wa Mkoa wa Mtwara,
Gelasius Byakanwa amesema katika ziara hiyo Rais Magufuli atazindua na
kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo.
Amesema
ataweka jiwe la msingi la upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mtwara na
lingine la ujenzi wa barabara ya Mtwara-Mnivata (Km 50),pia ataweka jiwe
la msingi kwenye kiwanda cha kubangua korosho cha Yalin kilichopo
Msijute na ataweka pia jiwe la msingi katika chuo cha ualimu cha
Kitangali.
Mh.Byakanwa
amesema licha ya kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali, Rais
Magufuli atazindua kituo cha afya cha Mbonde wilayani Masasi na barabara
ya Mangaka-Mtambaswala na pia Mangaka -Nakapanya iliyojengwa kwa
kiwango cha lami.
"Miradi
inayozinduliwa ni mikubwa ambayo itasaidia kuchochea kukua kwa uchumi
wa Mtwara na kwa uchumi wa Mtwara na nchi kwa ujumla na pia ni miradi
ambayo kwa Mtwara ina tija kubwa sana, hivyo amewaomba wananchi
wajitokeze kwa wingi katika maeneo yote yenye miradi ya maendeleo
itakayozinduliwa ili kumsikiliza Mh.Rais" amesema Mkuu wa mkoa huyo wa
Mtwara.
Hii
ni ziara ya pili kwa Rais Magufuli kutembelea Mkoa wa Mtwara tangu
alipoapishwa kuwa Rais mwaka 2015, ambapo safari hii anatarajia
kuzunguka katika wilaya zote za Mkoa huu.
Comments
Post a Comment