Rais Magufuli amekutana na kufanya
mazungumzo na timu ya wataalamu wa Tanzania na Misri wanaoshughulikia
ujenzi wa uwanja wa michezo katika Jiji la Dodoma, unaotarajiwa kujengwa
kwa msaada wa Mfalme wa Morocco Mtukufu Mohammed VI.
Balozi wa Morocco hapa nchini
aliyeongoza ujumbe wa wataalamu kutoka Morocco Abdelilah Benryane
amesema pamoja na kuzungumzia uhusiano mzuri wa Tanzania na Morocoo
wamejadiliana kuhusu utekelezaji wa miradi iliyokubaliwa wakati wa ziara
ya Mfalme wa Morocco hapa nchini mwaka 2016 ikiwemo ujenzi wa Msikiti
wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa Jijini DSM na kuanza
kwa ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu Jijini Dodoma.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara
Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale amesema uwanja huo
utajengwa eneo la Nanenane kando ya barabara ya Dodoma – Morogoro,
utajengwa kwa mfano wa mlima Kilimanjaro na utakuwa na uwezo wa kuchukua
watazamaji kati ya 85,000 na 100,005.
Comments
Post a Comment