President JPM ateua Manaibu Katibu Wakuu wawili wa Wizara ya Fedha na TRA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Adolf Hyasinth Mohondela Ndunguru kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango anayeshughulikia Sera.
Ndunguru ameteuliwa kushika nafasi ya Naibu  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango (Sera) ambayo ilikuwa wazi.
Kabla ya uteuzi huo Ndunguru alikuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Kufuatia Uteuzi huo, Rais Magufuli amemteua Msafiri Lameck Mbibo kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa TRA.
Kabla ya Uteuzi huo Mbibo alikuwa Meneja wa TRA Mkoa wa Kilimanjaro.
Uteuzi wa viongozi hao unaanza mara moja leo tarehe 31 Machi, 2019.

Comments