
Mama aitwaye Evelyn Namukhula mwenye umri wa miaka 28 amejifungua salama watoto watano katika Hospitali Kuu ya Kakamega nchini Kenya.
Evelyn Namukhula amejifungua kupitia njia ya upasuaji, ambapo madaktari wamethibitisha hali ya afya ya watoto wake ni nzuri.
Amejifungua wasichana watatu na wavulana wawili.
Kabla ya kujifungua, Namukhula alikuwa
na watoto wanne anaoishi nao na baba yao Herbert Nabwire katika kijiji
cha Sisokhe, eneo bunge la Navakholo.
"Namshukuru Mungu kwa mujiza huu. Hata
hivyo, nawaomba wahisani kujitokeza kwa kuwa sitakuwa na uwezo wa
kuwalea pekee yangu," alisema.
Comments
Post a Comment