Kamati ya Bunge yaridhishwa na juhudi za Wizara ya Madini


Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati) akikagua na kutoa maelekezo kwa Meja Atupele Mwamfupe ambaye ni Meneja wa Ujenzi SUMA JKT Kanda ya Kusini (kulia). Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Utawala na Raslimali watu wa Wizara ya Madini, Issa Nchasi.
Meneja wa Kanda ya Ujenzi SUMA JKT, Meja Atupele Mwamfup akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa kituo na kutafsiri michoro mbalimbali ya jengo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Raslimali Watu Wizara ya Madini Issa Nchasi, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, Makamu Mwenyekiti Mhe. Mriam Mzuzuri na wajumbe wengine.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akitoa maelezo ya ujenzi wa kituo cha umahiri Songea kwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, Mariam Mzuzuri (kushoto kwake). Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Raslimali Watu Wizara ya Madini, Issa Nchasi na Meja Atupele Mwamfupe ambaye ni Meneja wa Ujenzi SUMA JKT Kanda ya Kusini.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mariam Mzuzuri akimueleza jambo Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo baada ya kukagua ujenzi wa kituo cha umairi.

Na Issa Mtuwa, Songea
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mariam Ditopile Mzuzuri amesema kamati yake inaipongeza na itaendelea kuiunga mkono Wizara ya Madini kwa kazi nzuri inayofanywa na wizara hiyo.

Akiongea na waandishi wa habari mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, mjini Songea baada ya kukagua ujenzi wa kituo cha umahiri (Centre of excellence) kwa mkoa wa ruvuma, Mzuzuri aLIsema kamati yake inaridhishwa na kazi za Wizara ya Madini na wataendelea kuiunga mkono hasa sUala la wachimbaji wadogo.

"Tunawapongeza sana Wizara ya Madini, mnafanya kazi nzuri na sisi kama kamati niseme tutaendelea kuwaunga mkono hasa hili la wachimbaji wadogo". Alisema Mzuzuri.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo aliiambia kamati kuwa wizara yake imejipanga katika kukamilisha ujenzi wa vituo vyote vya umairi kikiwemo cha Songea kwa kuzingatia ubora. Alisema ujenzi wa vituo vyote unakwenda vizuri, hata hivyo kituo cha Songea kilichelewa ujenzi wake tofauti na vituo vingine kwa sababu mbalimbali ikiwemo uhaba wa upatikanaji wa kokoto changamoto ambayo imetatuliwa na kwa sasa ujenzi unaendelea kwa kasi.

"Wizara imekusudia kukamilisha ujenzi wa kituo hiki na vingine kwa wakati na kama nilivyo tangulia kusema zile changamoto zimesha tatuliwa na tuaendelea vizuri. Naishukuru kamati yako kwa kutuunga mkono na ushauri wote uliotolewa tutauzingatia". Alisema Nyongo.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa Ruvuma, Profesa Riziki Shemdoe akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo, aliwaambia wajumbe wa kamati kuwa ni kweli kuna kipindi mkoa wa Ruvuma ulikumbwa na changamoto ya upatikanaji wa kokoto na miradi mingi ya serikali ilisimama kutokana na kuwa na kampuni moja tu ya uzalishaji wa kokoto mkoa nzima, baada ya mitambo yake kuharibika na uzalishaji kusimama upatikanaji wa kokoto ulikuwa ni tatiizo.

Kituo cha Umahiri Songea ni miongoni mwa vituo mbalimbali vinavyo jengwa hapa nchini katika maeneo mbalimbali kama vile Bukoba, Simiyu, Tanga, Chunya kwa lengo la kuwasaidia wachimbaji wadogo kujifunza na kupata uelewa wa masuala mbalimbali ya madini.

Comments