
Uwezo wa kuwa na raha, maumivu na hofu si binadamu pekee wamaokuwa nao.
Ukweli ni kwamba uwezo huu wanao wanyama wa jamii mbali mbali.
Lakini ni vipi kuhusu hisia mbaya kama vile kuomboleza kifo cha mpendwa au kuhisi hasira wakati unapokosa kutendewa haki ?
Mapinduzi ya kibaiolojia na tabia pamoja na sayansi ya ubongo yamebaini
kuwa mifumo yetu ya neva inafanana sana na ile ya baadhi ya wanyama,
hasa wale wa jamii ya mamalia.
Sawia na hayo, baadhi ya hisia ambazo mara nyingi tunafikiri ni za binadamu si zetu peke yetu.
Ifuatayo ni mifano mitano iliyochukuliwa kutoka kwneye kitabu "The
Emotional Intelligence of Animals", kilichoandikwa na mtaalamu wa tabia
za wanyama Muhispania Pablo Herreros.
1. Hisia ya kutendewa haki
usipomtendea haki nyani aina ya capuchin tegemea kukabiliana na hasira yake

Watu wengi wanaweza kutofautisha kati ya wanapotendewa haki na pale
ambapo hawajatendewa haki. Nyani aina ya capuchin pia ana utambuzi huu.
Katika utafiti uliofanyw ana kituo cha Yerkes cha Atlanta, wanayama hawa
waligoma kuonyesha ushirikiano na watafiti walipohisi kuwa
hawakutendewa haki.
Watafiti walilipatia kundi la nyani aina ya capuchin vipande vya matango badala ya vipande vya plastiki.
lakini wakampatia nyani mmoja wao zabibu- chakula wanachokipenda sana.
baada ya kufanya hivyo mara, waliosalia wakagoma kuendelea kufanyiwa
uchunguzi. baadhi yao hata waliwarushia vipande vya matango biandamu.
2. Nia ya kulipiza kisasi
Ndovu wamekuwa wakifahamika kwa ulipizaji kisasi dhidi ya watu

Karibu sote binadamu wakati mmoja tumekuwa na hisia ya kulipiza kisasi
wakati mmoja. Ni kwa nini binadamu wasiwe na hisia sawa na sisi?
Mwaka 2016 kundi la tembo waliuvamia mji wa Ranchi, uliopo mashariki mwa
India, na kuwalazimisha wakazi kutoroka makazi yao ili kuokoa maisha
yao. Wanyama hao walikuwa wakiusaka mwili wa ndovu jike aliyekuwa
amekufa baada ya kuanguka kwenye mfereji wa maji ya umwagiliaji wa
mashamba.
Wanyama wnaweza kuonyesha hasira na ulipizaji wa kisasi dhidi ya watu wanaowatunza.
Na sokwe hukumbuka ni nani ni marafiki na ni nani ni maadui zao. Wakati adui anapomshambulia rafiki, wanaweza kulipiza kisasi.
3. Upendo wa mama
Upendo wa sokwe ambaye ni mama kwa mwanae unaweza kuwa ni thabiti

Binadamu huwa wanakuwa na upendo na kuwajali vizazi vyao. Lakini pia
wanyama wengine wana uwezo wa kuonyesha upendo sawa na huo wa mzazi kwa
mwanae.
Christina,sokwe kutoka Tanzania, alionyesha upendo hata kwa mwanae
ambaye alizaliwa na ugonjwa wa Down syndromena ngiri uliomzuwia kukaa
chini.
Watafiti kutoka katika chuo kikuu cha Tokyo walishuhudia namna wakati mwingine mama anavyoweza kuacha kula ili kumjali mwanae.
hakutaka yeyote ambebe mwanae wa kike, kana kwamba alifahamu kuwa hakuna
anayeweza kumjali mwanae kuliko yeye. Mtoto huyo wa kike alikufa akiwa
na umri wa miaka miwili.
Pablo Herreros pia aliandika kuhusu mama wa ndovu aambaye alitenganishwa
na mwanae ambaye alifunzwa na kuwaburudisha watalii nchini Thailand.
Miaka mitatu baadae, baada ya juhudi za wahifadhi wa wanyamapori
kumtafuta mwana wa tembo huyo, waliungana tena katika makazi ya tembo .
Mama na mwanae walisimama wima kwa saa nzima . Wakaanza kugusanisha
pe,mbe zao huku kila mmoja akimtomasa mwenzake.
4. Kuvunjika moyo
Ndege aina ya Macaw wanaweza kufa kwa kuvunjika moyo

Kuvunjika kwa uhusiano wa kimapenzi huwafanya watu waumie sana.
Ndege aina ya Macaw ambao ni waaminifu sana kwa wapenzi wao katika
kipindi chote cha maisha yao, huwa wanaumia sana wanapowapoteza wapenzi
wao.
Pale mmoja kati ya wapenzi anapokufa ghafla , mwingine huwa anapata
ugumu wa kuishi peke yake: mara nyingi huwa aliyebaki anashindwa kula na
kuwa dhaifu sana.
baadhi huwa dhaifu kiasi cha nkushindwa kuishi kwenye viota vyao na
kuanguka chini kwenye miamba. Ni kama aina fulani ya kifo cha mapenzi ?
5. Huruma na faraja
Panya buku wanauwezo wa kufarijiana

Binadamu wanauwezo wa kuwafariji binadamu wenzao na kuhisi kuwahurumia.
Mwaka 2016 utafiti uliochapishwa kwenye jarida la kisayansi ulibaini
kuwa panya hawa huwa wanawafariji wenzao wanaohisi msongo wa jambo
fulani , jambo ambalo watafiti wanalielezea kama ushahidi wa huruma.
Katika vipimo vya uchunguzi, panya wawili walitenganishwa. mmoja wao alipigwa na umeme kidogo.
Walipokutanishwa tena, panya ambaye hakupigwa na umeme alijaribu
kumfariji mwenzake kwa kumlamba kwa muda mrefu kuliko wanyama
wenginekatika kikundi ambao walikuwa pia wametenganishwa na ambao
hawakupigwa na nguvu ya umeme.
Kwa mujibu wanasayansi hii inaonyesha faraja kwa inayosaidia kuondoa
msongo kwenye ubongo jambo linalosaidia kuachiliwa kwa homoni za ubongo
zinazofahamika kama "homoni za upendo " - ambazo huboresha maisha yao.
Tafiti nyingine zimebaini kuwa sokwe, ndovu na mbwa huwafariji waathiriwa wenzao wa mashambulio.
Comments
Post a Comment