DRC yafanya uchaguzi wa maseneta. Maseneta 100 wamechaguliwa katika majimbo 24 ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Kila jimbo limewachagua maseneta 4 na jimbo la Kinshasa maseneta 8.
Uchaguzi wa Baraza la Seneti umefanyika leo Ijumaa katika Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo. Uchaguzi huo unawahusisha jumla ya maseneta mia
moja na nane kutoka kwenye majimbo yote ya nchi hiyo. Uchaguzi huo
unafanyika kukiwa na lawama za ushawishi wa kikabila.
Kwa fursa
hii ni maseneta mia moja waliochaguliwa katika majimbo ishirini na nne
ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Kila jimbo limewachagua maseneta
wanne na jimbo la Kinshasa maseneta wanane. Hata hivyo, hadi sasa, bado
uchaguzi wa wabunge haujafanyika katika majimbo ya Kivu Kaskazini na
Maindombe, ambako maseneta wengine wanane watatoka huko.
Katika Kivu
Kusini, Pierre Lumbi, akiwa mgombea wa chama cha Lamuka cha Martin
Fayulu amechaguliwa, na wagombea watatu wengine ni kutoka muungano wa
FCC unaovihusisha vyama vinavyomuunga mkono rais aliyeondoka madarakani
Joseph Kabila.
Uchaguzi wa maseneta unafanyika wakati huu kukiwa
na baadhi ya wakaazi wa Kivu Kusini kutoka kabila za "Balega”,
wanaonyoosha kidole cha lawama kuhusu uchochezi wa ukabila katika
harakati zote za uchaguzi tangu Desemba 30. Na kama inavyoonekana kwa
mara nyingine tena, hakuna mtu wa kabila hilo aliyechaguliwa.
Miongoni
mwa viongozi wa kabila hili wanaokerwa na suala hilo ni pamoja na
Jean-Marie Bulambo Kilosho, mbunge wa kitaifa ambaye kwa sasa yuko
ziarani mjini Bukavu. Kilosho anahisi kwamba baadhi ya wabunge
wameshawishiwa na viongozi walioko Kinshasa.
Hali hii
imesababisha baadhi ya vijana wa kabila hili la Balega kuonesha nia yao
ya kulitaka jimbo hili la Kivu Kusini ambapo tayari zaidi ya saini laki
moja na themani na sita zimekusanywa, kwa lengo la kuibadili hali
iliyopo. Mbunge Bulambo Kilosho anafafanua zaidi.
Ombi hili
linatupiliwa mbali na asasi nyingi za kiraia hapa Kivu Kusini. Zozo
Sakali ni mwanasheria na pia kiongozi wa asasi ya kiraia mjini Bukavu.
Baada ya uchaguzi huu wa maseneta, uchaguzi wa magavana wa majimbo unapangwa kufanyika Machi 26.
Comments
Post a Comment