
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi
(CCM), Dk Bashiru Ally, amewataka wanachama wa CCM kuheshimu alama za
vyama vyote vya siasa nchini kwa sababu vimesajiliwa kisheria.
Dk Bashiru amesema hayo wakati akizindua mkakati wa kukomaza demokrasia kwenye mashina ulioandaliwa na CCM mkoa wa Dodoma.
Amewataka kutochoma wala kubeza alama za
vyama hivyo na kwamba huku akigusia suala la wafuasi wengine kuchoma
bendera na kupaka rangi ya chama chao ofisi za chama kingine.
"CCM tusifanye mambo holela na uhuni huo
katika siasa. Ni kosa kuparamia na kupaka rangi ofisi za vyama hivyo.
CCM tusifanye hivyo ni kosa kisheria''. amesema.
Ameongeza, Sisi wanachama wa Chama cha
Mapinduzi tunao wajibu wa kulinda uhuru wa vyama vingine vilivyosajiliwa
kisheria, kama sisi tunafurahi na kuimba nyimbo zetu acheni na wao
wafurahi na kuimba nyimbo zao, kama sisi tunapendeza na nguo zetu acheni
na wao wapendeze na nguo zao.
Chanzo - EATV
Comments
Post a Comment