Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe. Said
Nkumba tarehe 15 Machi, 2019 amekabidhi rasmi vifaa tiba vyenye thamani
ya Tsh. Million 20,540,000/= vilivyotolewa na Mhe. Doto Biteko Mbunge
wa Jimbo la Bukombe wakati wa uzinduzi wa Zahanati ya Msasani iliyopo
kata ya Bugelenga.
Nkumba alisema “vifaa tiba ambavyo
vimetolewa na Mhe. Biteko navikabidhi rasmi kwenye Zahanati hii ili
viweze kuwapunguzia hadha wananchi wa kijiji cha Msasani hasa akinamama
wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano waliokuwa
wanalazimika kwenda kijiji cha Bugelenga kwa ajili ya kupatiwa huduma za
afya”.
Aidha Nkumba ametoa wito kwa Diwani wa
kata ya Bugelenda Mhe. Baraka Hussain kuhakikisha anakilea kituo hicho.
”Mh. Baraka hakikisha unakilea kituo hiki na usisubiri kuitwa, hakikisha
unakuja kila wakati kuangalia zoezi zima la utoaji wa huduma
linavyoendelea.”
Pia amewataka wanachi wa kata ya
Bugelenga kuhakikisha wanashiriki shughuli za maendeleo kikamilifu ili
waweze kupata fedha za serikali zitakazosaidia katika ukamilishaji wa
majengo yao kwani bila kufanya hivyo hakuna fedha yoyote ya serikali
itakayotolewa bila ya uwepo ya nguvu zozote za wananchi.
Naye Mhe. Baraka amemshukuru Mhe.
Biteko, uongozi wa Halmashauri pamoja na wananchi kwa kuhakikisha
Zahanati hiyo inaanza kutumika kama ilivyokusudiwa.
Comments
Post a Comment