
Mamlaka hiyo imesema mapema Jumatatu,
Februari 11 kuwa imeliagiza Shirika la Ndege la China kusitisha matumizi
ya ndege za Boeing 737 hadi hapo itakapotoa taarifa zaidi kuhusu
kurejea kwa safari zake.
Ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia
aina ya 737 MAX 8 ilipata ajali dakika chache baada ya kuruka katika
Uwanja wa Ndege wa Addis Ababa Jumapili, March 10.
Hiyo ni ajali ya pili ya ndege hizo
ambazo ni toleo jipya la kampuni ya Boeing lililotolewa mwaka 2017,
ambapo mnamo Oktoba mwaka 2018, ndege ya Shirika la Ndege la Indonesia
iliyokuwa ikifanya safari za ndani ilianguka dakika 13 baada ya kuruka
kutoka Uwanja wa Ndege wa Jarkata na kuua abiria 189 pamoja na wahudumu
wa ndege.
Shirika la Ndege la China linamiliki
jumla ya ndege 96 aina ya Boeng 737 MAX, ambapo imesema imeona mfululizo
wa vyanzo vya ajali za ndege hizo zinafanana.
Lakini msemaji wa Shirika la Ndege la
Boeing ameuambia mtandao wa Reuters akikanusha tuhuma hizo za China,
akisema kuwa hana uhakika na taarifa ambazo nchi hiyo inazitumia.
Comments
Post a Comment