Ripoti
17 za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa
Mussa Assad, kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2018 zimekabidhiwa
rasmi kwa Rais Dk. John Magufuli.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar es Salaam na Ofisi ya Taifa ya
Ukaguzi (NAOT), ripoti hiyo imewasilishwa na CAG katika hafla fupi
iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam juzi na kuhudhuriwa na viongozi
mbalimbali kutoka ofisi hiyo.
CAG
alimkabidhi Magufuli ripoti ya Ukaguzi wa Serikali Kuu, Ripoti ya
Ukaguzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Ripoti ya Ukaguzi wa Mashirika
ya Umma na Ripoti ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo.
Pia
alikabidhi Ripoti ya Ukaguzi wa Mifumo ya Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano, Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi na ripoti 11 za ukaguzi wa
ufanisi katika sekta mbalimbali.
Sekta
hizo ni pamoja na usimamizi wa shughuli za ujenzi wa miradi ya
umwagiliaji, usimamizi wa miradi ya maji vijijini, usimamizi wa miradi
ya maji itokanayo na visima virefu.
Nyingine
ni matengenezo ya mitambo ya kuzalisha umeme, usimamizi wa elimu kwa
wanafunzi wenye mahitaji maalumu, usimamizi wa mfumo wa ununuzi wa
magari ya Serikali kwa pamoja pia sekta ya ufuatiliaji wa shughuli za
ujenzi na majengo ya mijini, usimamizi wa utoaji wa huduma za afya za
rufaa na dharura kwa hospitali za rufaa ngazi ya juu, upatikanaji na
usambazaji wa pembejeo za kilimo, usimamizi wa utoaji wa huduma ya bima
ya afya na ufuatiliaji wa mapendekezo ya ukaguzi wa ufanisi.
Akizungumza
baada ya kupokea ripoti hiyo, Magufuli aliipongeza ofisi ya CAG kwa
kazi nzuri inayofanya na pia kuahidi kuwa Serikali itaendelea
kushirikiana nao kwa karibu na katika kukabiliana na kudhibiti matumizi
mabaya na upotevu wa fedha za umma.
Comments
Post a Comment