Taarifa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Jana March 27, 2019 inatuambia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Richard Faustine Sambaiga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Dkt. Sambaiga umeanza March 23, 2019.
Dkt. Sambaiga
ni Mhadhiri Mwandamizi, Idara ya Sosholojia ya Chuo Kikuu cha DSM na
anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Rukia Masasi ambaye amemaliza muda
wake.
Pia Rais Magufuli Leo March 28, 2019 atamuapisha Balozi Mteule Valentino Mlowola kuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba.
Balozi Mteule Mlowola ataapishwa Ikulu Jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 3:30 asubuhi.
Comments
Post a Comment