DC NKUMBA AWASISTIZA WANACCM KULINDA UHAI WA CHAMA HICHO

Mwenyekiti wa  CCM Wilaya ya Bukombe Daniel Machongo akitoa muongozo wa kikao kwa wajumbe wa halmashauri kuu YA CCM 

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba akitoa ufafanuzi juu ya taarifa ya utekelezaji wa miradi katika Wilaya ya Bukombe

Wajumbe wakiskiliza taarifa ya utekelezaji wa miradi katika Wilaya ya Bukombe


Mmoja ya wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Bukombe akitoa maoni juu ya taarifa ya utekelezaji wa miradi katika Wilaya ya Bukombe



Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mkoa wa Geita, Said Nkumba ametoa
wito kwa viongozi wa chama cha mapinduzi CCM kuanzia ngazi ya shina,
matawi kata hadi wilaya kuendeleza uhai wa chama.

Nkumba alisema Uhai wa mwanachama wa CCM haupatikani kwa kulipa ada tu
inatakiwa kuleta uhai kwa kushiriki kwenye miradi mbalimbali ya
maendeleo.

Alisema Serikali ya Wilaya ya Bukombe kwa kutekeleza Ilani ya CCM kuanzia
Julai hadi Desemba 2018 Pesa ya serikali iliyotolewa  kwa ajili ya miradi sh
2.6 bilioni iliyotumika sh 2.2 bilioni

Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Bukombe Jazaa Komba baada
ya kupokea taarifa hiyo walishauli serikali kuongeza vitabu
kunaupungufu mkubwa mashuleni na kukamilisha maboma ya miradi
iliyoibuliwa na wananchi kwa muda mrefu.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bukombe Daniel Machongo alimpongeza Mkuu
wa Wilaya ya Bukombe
Said Nkumba kwa kazi anazofanya kwa ajili ya maendeleo ya wananchi kwaa
kutekeleza ilani.

Machongo aliwaomba wananchama kushirikiana na serikali kuhakikisha
wananchi wanaibua miradi na serikali ilete fedha kwa ajili ya
ukamilishaji.


Comments