Balaa Kahama!! WANUSURIKA KUFA KWA KUBUGIA UNGA WA REMOTE NDUGU WAKITUHUMIANA KUCHEPUKIANA WAO KWA WAO
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao
Vijana wawili Rosemary Embasy (17) na
Yohana Petro (19) wamenusurika kufa baada ya kunywa vidonge vingi na
unga wa betri za remote na maji kutokana na mgogoro wa mapenzi
ulioigubika familia ya Petro Dalali (41) mkazi wa kijiji cha Mwime ya
Ilindi kata ya Zongomela wilayani Kahama. Anaripoti Kadama Malunde.
Kwa Mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Shinyanga ACP Richard Abwao tukio hilo limetokea Machi 18,2019 majira ya
saa ya saa tisa alasiri Kijiji cha Mwime ya Ilindi.
Akisimulia kuhusu tukio hilo,Kamanda
Abwao amesema siku ya tukio hilo, binti aitwaye Rosemary Embasy (17)
mkazi wa Mwime alijaribu kujiua kwa kunywa vidonge vingi pamoja na unga
wa betri za remote uliochanganywa na maji baada ya kumuona mtoto wa mama
yake mkubwa aitwaye Yohana Petro (19) na yeye amekunywa vidonge vingi
kwa lengo la kujiua.
“Chanzo inadaiwa kuwa wazazi wa
Yohana Petro wamekuwa na mgogoro ambapo mama yake aitwaye Magdalena
Lucas (39), amekuwa akimtuhumu mtoto wa mdogo wake yaani Rosemary Embasy
kuwa ana mahusiano ya kimapenzi na mume wake . Pia baba yake Yohana
Petro aitwaye Petro Dalali (41 amekuwa akimtuhumu mtoto wake Yohana
Petro kuwa anatoka kimapenzi na Rosemary Embasy ambaye ni mtoto wa
shemeji yake”,
“Ndipo tarehe 18/03/2019 majira ya
saa nne asubuhi Yohana Petro alifika nyumbani kwa Rosemary Embasy na
kuingia ndani kisha kunywa vidonge vingi ambapo Rosemary Embasy baada ya
kuona hivyo na yeye alimeza vidonge vilivyobaki na kuponda unga wa
betri ndogo kisha kunywa pamoja na maji”,ameeleza Kamanda Abwao.
Amesema tayari baba wa familia Petro
Dalali na mkewe aitwaye Magdalena Lucas, na Dominic Magoha (31)
wanashikiliwa kwa mahojiano zaidi.
Aidha amesema Rosemary Embasy na Yohana
Petro wanaendelea na matibabu hospitali ya Halmashauri Mji wa Kahama
wakiwa chini ya ulinzi na hali zao zinaendelea vizuri.
Kamanda Abwao ametoa wito kwa wananchi,
pale inapotokea migogoro ama matatizo ya kifamilia kutojichukulia
maamuzi ya kujidhuru, kwani ni kosa kisheria, badala yake waripoti kwa
mamlaka za kisheria/ kiushauri ili kutatua matatizo yanayotokea.
Comments
Post a Comment