Waziri wa Madini, Doto Biteko leo tarehe 06 Februari, 2019
amekutana na watendaji na watumishi wa Tume ya Madini katika makao makuu ya
Tume yaliyopo jijini Dodoma, lengo likiwa ni kusikiliza na kutatua changamoto
mbalimbali zinazoikabili Tume.
Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati) akisikiliza
mapendekezo mbalimbali yaliyokuwa yanawasilishwa na watumishi wa Tume ya Madini
(hawapo pichani)
Kikao hicho
kilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon
Msanjila, Mkurugenzi wa Utawala na
Usimamizi wa Rasilimaliwatu kutoka Wizara ya Madini, Issa Nchasi na Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris
Kikula.
Wengine ni pamoja na Kamishna kutoka Tume ya Madini, Dkt.
Athanas Macheyeki, Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya,
Wakurugenzi, Mameneja pamoja na watumishi wa
Tume ya Madini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila
akifafanua jambo katika kikao hicho.
Katika kikao hicho Waziri Biteko ametoa maelekezo mbalimbali
ikiwa ni pamoja na vituo vya ukaguzi wa madini ya ujenzi kufufuliwa, kikao cha
kamati tendaji kukutana mara kwa mara kwa ajili ya kupitia na kuidhinisha
maombi mbalimbali ya leseni za madini na watumishi kufanya kazi kwa uadilifu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila
akifafanua jambo katika kikao hicho.

Kutoka kushoto, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa
Simon Msanjila, Waziri wa Madini, Doto Biteko na Mwenyekiti wa Tume ya Madini,
Profesa Idris Kikula wakifuatilia hoja mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa na
wafanyakazi wa Tume.
Watumishi wa Tume ya Madini wakifuatilia hotuba iliyokuwa
inatolewa na Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani)
Comments
Post a Comment