Waziri wa Madini, Doto Biteko (pichani) amefungua warsha ya siku mbili
kuanzia leo Februari 11, 2019 kwa wadau wa madini inayolenga kujadili
maudhui ya kanuni mpya za uanzishwaji masoko ya madini kama alivyoagiza
Rais Dkt. John Pombe Magufuli hivi karibuni.
Warsha hiyo inayofanyika Jijini Mwanza imeandaliwa na Wizara ya Madini
kupitia uratibu wa taasisi ya Uongozi Institute na kuwashirikisha wadau
na viongozi mbalimbali kutoka mikoa 12 nchini.
Waziri wa Madini, Doto Biteko (wa watu kushoto waliokaa) akiwa kwenye
picha ya pamoja na viongozi mbalimali akiwemo Katibu Mkuu Tume ya
Madini, Profesa Simon Msanjila, (wa pili kushoto waliokaa), Kamishna wa
Madini, Mhandisi David Mulabwa (wa kwanza kushoto waliokaa) na Wakuu wa
Wilaya zilizoshiriki warsha hiyo.
Wengine waliokaa ni Mkuu wa Wilaya Misungwi, Juma Sweda (wa pili kulia)
aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Mwanza pamoja na Mkuu wa Idara ya Mafunzo
kwa Viongozi kutoka taasisi ya UONGOZI Institute, Kadari Singo (wa
kwanza kulia) aliyemwakilisha Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo.
Waziri wa Madini, Doto Biteko akiwa kwenye picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Halmashari za Wilaya zilizoshiriki warsha hiyo.
Waziri wa Madini, Doto Biteko akiwa kwenye picha ya pamoja na Makatibu Tawala kutoka wilaya zilizoshiriki warsha hiyo.
Waziri wa Madini, Doto Biteko akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa wizara hiyo.
Waziri wa Madini, Doto Biteko akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa wachimbaji wadogo wa madini.
Waziri wa Madini, Doto Biteko akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa taasisi ya UONGOZI Institute.
Comments
Post a Comment