VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA HIMIZENI NGUVU ZA JAMII KUTEKELEZA BAJETI


 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya  Bukombe Mhe. Safari Nikas Mayala akiendesha Baraza La Madiwani Katika Kikao cha Bajeti kwa mwaka wa Fedha 2019/2020

Afisa Utumishi Wilaya ya Bukombe Honorat Mtasingwa Akifafanua Jambo katika baraza la Madiwani 

 Waheshimiwa Madiwani wakionyesha Umakini mkubwa katika kufatilia Bajeti ya fedha 2019/2020


 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bukombe Daniel Machongo Akizungumza kwenye Baraza la Madiwani.

Viongozi Wa Vyama Vya Siasa Walioudhuria Katika Baraza la Madiwani

Viongozi wa vyama vya siasa Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita,
wametakiwa kuhimiza wananchi kutekeleza malengo ya serikali katika
kukusanya mapato ya ndani.

Wito huo ulitolewa na mwenyekiti wa halmashauri  Safari Mayala wakati
wa kupitia makisio ya mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2019/2020
aliwaomba watalamu na wanasiasa wanatakiwa  kushirikiana kuhamasisha
nguvu zaja ili waweze kutekeleza malengoyaserikali.
Mayala alisema iwapo tutatasasiri kuwa bajetihiyi ni ya CCM
tutachelewa kupata maendeleo badalayake tujielekeze kwa ushirikina
kuelimisha wananchi.


Awali Afisa Mipango Wilaya Sarah Yohana  aliliambia Baraza la Madiwani
kuwa makisio ya mpango wa na bajeti kwa mwaka wa fedha 2019/2020
halmashauri inatalajia kupokea jumla ya  sh 32.7 bilioni katika bajeti
hiyo mapato ya ndani sh 1.9 bilioni ruzukutoka serikali kuu sh 26.8
bilioni miradi ya maendeleo ruzuku na nguvu za kijamii imetegewa sh
3.8 bilioni.


Yohana alisema mwaka huu bajeti imeshuka ikiwa kwa mwaka wa fedha
2018/19 halmashauri ilipanga kutumia sh 36.7 bilioni yakiwemo makisio
ya makusanyo ya ndani sh 2.3 bilioni hadi  kufikia Desemba 31 mwaka
2018 halmashauri ilikuwa imepokea na kukusanya sh 11.6 bilioni na
zilizotumika ni sh 11.3 bilioni.


Mkurugenzi Mtendaji wa Halamshauri ya Wilaya ya Bukombe Dionis Myinga aliongeza kuwa
Madiwani wawe msitari wa mbele kuhamasisha wananchi kuelimisha jamii
katiika kulipa ushuru na kuhakikisha wanazingatia malekezo ya serikali
hasa kwenye malipo ya posho elekezi katika vikao ya madiwani na vikao
vya watumishi wahakikishe wanajibana ili wafikie malengo ya ukusanyaji
wa mapato ya ndani.


Comments