SERIKALI YAWATAKA WANANCHI KUANZISHA BIASHARA NDOGO NDOGO ZA KUTUMIA NISHATI

 Waziri Wa Nishati Dkt Medard Kalemani Akisalimiana Na Meneja wa Tanesco Wilaya ya Bukombe mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bukombe

  Waziri Wa Nishati Dkt Medard Kalemani akisalimiana na Wajumbe wa UWT alipowasili katika Ofisi ya CCM Wilaya ya Bukombe.


Mwenyekiti CCM Wila ya Bukombe Daniel Machongo akizungumza katika ugeni wa Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani baada ya kuwasili Ofisini hapo.



 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukombe Mhe. Safari Nikasi Mayala akizungumza na wananchi wa Kata ya Uyovu.
 Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba akizungumza na wananchi wa Kata ya Uyovu
 
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akiwasalimia wananchi kata ya Uyovu
 
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kaleman akikabidhi kifaa kiitwacho Umeme Tayari (UMETA) kwa Wazee wa Kata ya Uyovu.

 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akikabidhi Kifaa cha (UMETA) kwa mlemavu


Wananchi wa Kata ya Uyovu wakiwa mkutanoni

Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akikata utepe


 Serikali imewahimiza wananchi kuanzisha biashara ndogo ndogo
na kubwa ili kunufaika na Mradi wa umeme wa REA.


Wito huo ulitolewa na Waziri wa Nishati Dkt. Medard Karemani wakati akihutubia wananchi wa Kijiji cha Lyobahika Kata ya Uyovu Wilaya ya Bukombe mkoani Geita aliwaomba wananchi kuwa wavumilivu ambao hawaja washiwa umeme wakati serikali ikiendelea kumsukuma mkandarasa wa mradi asiruke kitongoji hata kimoja bila kuweka umeme.


Karemani alisema kunawananchi wanalilia umeme kwa ajili ya kuweka ndani
na kuwataka  kuondokana na dhana ya kuwa umeme huu ni kwa ajili ya mwanga tu bali  umeme ni frusa ya maendeleo wananchi wahakikishe wana anzisha biashara ndogo ndogo za ujasiliamali kwa kutumia umeme.


Karemani aliwataka maafisa wa Tanesco kupokea fedha za malipo kidogo kidogo toka kwa
wananchi kuanzia sh 2000 na kunatoa risti na mwananchi anapo kamirisha
sh 27000 afungiwe umeme.


Awali Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba alisema kwa mjibu wa sense ya watu na makazi 2012 Wilaya ina watu 224,542 kati yao wananufaika na mradi wa umeme wa tanesco 2015  mradi wa REA awamu ya tatu ulianza 2019 na utakamirika 2021 ambao unaendelea kutandazwa nguzo vijiji na
vitongoji 64 wateja 1358 wanatarajia kuunganishiwa umeme.


Nkumba alisema wateja wanaonufaika na mradi wa umeme 3931 kati yao wenye matumizi ya umeme madogo  976 wateja wa matumizi ya kawaida 2952 wateja wa matumizi ya kati 2 wateja wa umeme matumizi makubwa 1 na kuongeza iwapo mradi huu utakamirika wananchi watakuwa na frusa ya kiuchumi kupitia umeme kwa kufanya biashara ndogo ndogo za ujasiliamali ilikukuza pato la familia na taifa kwa ujumla.


Mjasiliamali kikiji cha Lyobahika Benjamini Mkandi alishukuru serikali kuwaletea umeme na kufafanua kuwa sasa ananufaika kwa kuunza vinywaji baridi zamani alikuwa naunza vinywajnakupata Tsh 7000 lakini saivi anauza hadi Tsh 20000 kwa siku.

Comments