SERIKALI YATOA TSH 325 MILIONI KUJENGA MADARASA


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Mh Safari Nikasi Mayala akiendesha kikao cha Baraza la Madiwani Katika ukumbi wa Halmashauri ya Bukombe.
 
Diwani wa Kata ya Bulangwa Mh Yusuph Mohamed akizungumza jambo katika kikao cha Baraza la Madiwani
 
Wenyeviti Wa Kamati wakiwa katika umakini wa kuskiliza mwenendo wa kikao cha Baraza la Madiwani


Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Bukombe wakifatilia kwa ukaribu kikao cha Baraza la Madiwani


 
Kaimu Mkurugezi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe
Mkoani Geita Joseph Machibya  alisema halmashauri imepokea Tsh milion 325
toka serikari  kuu kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma ya
madarasa ya shule za sekondari 13 kila shule imepangiwa Tsh milioni  25
ili kuondoa changamoto za upungufu wa vyumba vya madarasa.

Machibya aliyasema hayo kwenye Baraza la Madiwani wakati akitoa
taarifa ya Halmashauri ilivyo pokea fedha toka serikali kuu kwa
maelekezo ya miradi ya maendeleo.

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Said Nkumba aliwaomba kutotumia fedha hizo kwa
matumizi mabaya na kusisitiza  zisianze kutumika bila nguvu za wananchi kwanza,
aliwaomba madiwani kuhamasisha wananchi kuchangia nguvu zao kwa
kuchimba msingi, kusomba mchanga, na maji na vitu vingine ambavyo siyo
vya dukani.

Nkumba aliwaomba wazazi na walezi kutowa taarifa kwenye Ofisi za Serikali
wanapo ona watoto wao wanamimba na kwamba asiwepo Mtendaji wa Kijiji
na Kata kumaliza maswala ya mimba kwa mwanafunzi ofisini kwao badala yake
kesi za mimba zifikishwe polisi na ngazi zingine za juu.

  Afisa Elimu Vifaa na Takwimu shule za sekondari Wilaya Leonard Nkingwa
 alisema wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza 2019
ni wanafunzi 4477 mpaka Februari 28 mwaka 2019 wameripoti wanafunzi
4209 sawa na asilimia 94 ambao hawajaripoti wanafunzi 208 sawa na
asilimia 6.

Nkingwa alisema kunachangamoto ya upungufu wa madarasa na kwamba
serikali imeleta fedha za ukamilishaji wa maboma shule za sekondari na
Wilaya ina shule za sekondari 18 ikiwa za binafisi 3.

Awali walimu wa shule ya msingi Azimio Kata ya Katente Wilaya hapa
iliyoshika nafasi ya kwanza Wilayani Bukombe wanatamani kushika nafasi
ya kwanza kimkoa au Taifa.

Hayo yalielezwa na mwalimu wa taluma Savera Mkama akiwa anapokea hati
ya pongezi ya ufaulu na kushika nafasi ya kwanza kiwilaya kati ya
shule 78  kwa niamba ya mkuu wa shule ya msingi Azimio kwenye Baraza
la Madiwani wa Halmashauri ya Bukombe.

Mkama alisema mikakati ya kuwafanya wawe wakwanza kiwilaya ni kufanya
mitihani ya majalibio kwa wanafunzi kila mwezi na mitihani ya ujilani
mwema ikiwemo ya moko lakini mwaka huu wamejiwekea mikakati ya
wanafunzi kufanya mitihani ya mara kwa mara  ya ndani kila wiki ili
kuitafuta nafasi ya kwanza kimkoa inagwa malengo nikuwa wakanza
kitaifa.

Alisema changamoto alisema ni ukosefu wa umeme kwa ajili ya kuandaa
mitihani na wamekuwa wakitumia gharama kubwa kutumia Jenereta na kwamba
serikali iwaongezee mishahara na kulipa mapunjo yao na wamekuwa
hawapewi feddha za  likizo kwa wakati  hali ambayo ni changamoto kwao.

Mwalimu wa shule ya msingi Uyovu Severine Jegu ambaye shule yake
imeshika nafasi ya tatu kiwilaya na pia nafasi ya 20 kati ya shule
zilizofanya vizuri kitaifa alisema wamekuwa wakishirikisha wazazi na
walimu kutumia muda wa ziada kufundisha darasa la saba.

Afisa Elimu Taluma Shule za Msingi Wilaya Kassim  Mussa   alisema
katika matokeo ya kumaliza Elimu ya msingi 2018 Halmashauri ya Bukombe
imeshika nafasi ya  22 kitaifa kati ya halmashauri 186 kitaifa kimkoa
Bukombe imeshika nafasi ya 2 kati ya halmashauri 6 ufaulu ulikuwa ni
asilimia 86.82 jumula ya watahiniwa walikuwa 5008  wavulana 2433
wasichana 2575  waliofaulu wasichana 2283 wavulana  2215  jumula ya
wanafunzi waliofaulu 4498 kati ya shule za msingi 78 waliofeli ni
wanafunzi 510.

Mussa alisema serikali inashugulikia changamoto za walimu na kwamba
hakuna mwalimu anae cheleweshiwa fedha za kwenda likizo aliwaomba
walimu kuwa wavumilivu na kutambua kuwa taluma ya uwalimu ni wito
wahakikishe wanajituma kufundisha.

Wakati akikabizi hati za pongezi kwa shule 10 zilizofanya vizuri kati
ya shule 78 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Safari
Nikas Mayala aliwaomba walimu kuendelea na mikakati yao na kwamba wasibweteke
na hati au pongezi badala yake waendelee kuwa wabunifu ili kufikia
malengo yao na kwamba kwa kikao cha baraza cha kufunga mwaka wa fedha
2018/19 wataanda kinyango kwa shule ya mwisho kama zawadi.

Comments