Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack (kulia)
mara baada ya kuwasili katika kituo cha afya Samuye mkoani Shinyanga.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kulia)
mara baada ya kuwasili katika kituo cha afya Samuye mkoani Shinyanga.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
amewasili mkoani Shinyanga tayari kwa ziara ya kikazi ya siku 5.
Makamu
wa Rais ambaye amesafiri kwa njia ya barabara akitokea mkoani Tabora
ambapo napo alikuwa na ziara yenye lengo la kuhamasisha na kukagua
shughuli za kimaendeleo.
Mara
baada ya kuwasili mkoani Shinyanga Makamu wa Rais alitembelea kituo cha
Afya cha Samuye na kupata nafasi ya kuzungumza na wananchi wa eneo hilo.
“Serikali ina kila nia ya kusogeza huduma za afya bora kwa wananchi”alisema Makamu wa Rais.
Aidha
aliwaambia wananchi hao kuwa Serikali inakuja na sheria ya mpango wa
bima za afya kwa wote ambayo itamuhitaji kila mtanzania kuwa na bima ya
afya.
Makamu
wa Rais amewataka wakazi wa kata ya Samuye kushirikiana katika kuzuia
mimba za utotoni kwani kwa kiasi kikubwa zinahatarisha maisha ya watoto
wa kike.
Kwa
upande wake Naibu Waziri TAMISEMI Mhe. Mwita Waitara amesisitiza
Halmashuri kutenga asilimia 40 kwa ajili ya miradi ya maendeleo na
kuzitaka halmashauri zote kumalizia maboma ya zahanati wakati serikali
kuu inaleta pesa za kumalizia maboma ya shule na madawati.
Comments
Post a Comment