Viongozi wa chama na serikali watakiwa kuweka maslahi ya Taifa mbele kwa kuacha ubinafsi ili kutengeneza nchi bora isiyo na mafisadi pamoja na wala rushwa
Wito huo umetolewa na mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Geita Alhaj Said Kalidushi wakati akizungumza na
Wanaccm Kata ya Igulwa Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita iliwa ni mwendelezo wa
ziara yake kwenye kata zote 17 za Wilaya hiyo.
Kalidushi alisema viongozi wengi
hawapendi kufanya kazi kwa hiari yao wanapenda kusumwa na kuwasihi kuiga mfano
kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanzania na Mwenyekiti wa Chama cha
Mapinduzi Taifa Dkt John Pombe Magufuli jinsi anavyojitoa kwa dhati juu ya Nchi
katika kuhakikisha inaendelea kukua kiuchumi na kuzidi hakikisha amani yetu
haipotei.
Aliwataka Wanaccm wa Wilaya Bukombe
na Geita kwa ujumla kuwa waadilifu kwa kumchagua kiongozi bila kutumia rushwa
na hatimae kupata kiongozi asiyekuwa na uwezo mzuri wa kuwahudumia wananchi na
kuachana na makundi baada ya uchaguzi ili kulinda heshima ya Chama Cha
Mapinduzi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Bukombe Daniel Machongo aliwataka Viongozi kujijengea
uwezo mkubwa wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua kwa wakati ili kuondoa
lawama zisizokuwa za lazima
Pia Katibu wa Itikadi na Uenezi
wa Wilaya ya Bukombe Ladislous Soku aliwasihi viongozi wa chama na serikali
kufanya kazi za wananchi bila ubaguzi ili kurahisisha utekelezaji wa ilani ya
Chama Cha Mapinduzi kwa haraka.
Comments
Post a Comment