Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba (pichani)
Wazazi na walezi Wilayani Bukombe Mkoani Geita, wametakiwa
kupeleka wanafunzi waliofauru kujiunga na masomo ya sekondari mwaka 2019 kabla
ya serikali kuwachukulia hatua za kisheria.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba
Ofisini kwake kutokana na kuwepo na baadhi ya wazazi na walezi kutopeleka wanafunzi
kwa wakati na kusababisha wanafunzi wengi kutoroka nyumbani na kujiingiza
kwenye vishawishi vya kuolewa, kufanya biashara ndogo ndogo na uchimbaji wa
madini.
“Hakuna kitu kinachokera kama wazazi wasiopenda kusomesha
watoto wao wakati serikali inatoa elimu bure
Wazazi wekezeni kwenye Elimu ili kutoa urithi wa kweli kwa
watoto.” Nkumba alisema.
Alisema amefanya ziara shule za sekondari na kukuta mwitikio
wa wazazi wa kupeleka wanafunzi shuleni ni mdogo hadi alipo anza kuhamasisha
viongozi wa vijiji na kata kuwashughulikia wazazi hali ambayo inaleta matumaini
hadi sasa.
Nkumba alisema serikali haiwezi kukubali ikiwa mikakati ya
serikali ya Wilaya ni kuanzisha kampeni ya kuhamasisha wazazi kusomesha watoto
na kuchukuliwa hatua kali kwa watakao
kuwa hawaja wapeleka watoto shuleni.
Nkumba alisema shule za sekondari Wilayani hapa ni 15 lakini
hadi Januari 16 mwaka huu inaonyesha takwimu ya wanafunzi walioripoti ni
3129 na 1325 hawajaripoti kati ya wanafunzi waliofaulu 4467 mwaka 2018.
Amewataka wananchi kuiunga mkono serikali ya awamu ya
tano kwa wazazi kuhakikisha wanatumia
frusa ya Elimu bure kuanzia chekechea hadi kidato cha nne kusomesha watoto wao
kwa kuwanunulia vifaa na sale za shule.
Ofisa mtendaji wa kata
ya Butinzya Pamba Mgabali alisema kwamba wananchi bado wanamwamko mdogo wa
kusomesha na kwamba kamati ya maendeleo ya kata
imekuwa ikihamasisha wazazi kupeleka wanafunzi shule na kuchangia mali
zao kuboresha miundombinu ya shule.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya sekondari Butinzya Sayi Gibe
alianza kwa kumshukuru Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba kwa kuchukua hatua
za haraka kuanza ziara vijijni kwenda anahamasisha wazazi na walezi kuwapeleka
watoto wao shuleni hali ambayo imeleta matokeo makubwa ya kuripoti wanafunzi
kwa wingi.
Mwanafunzi wa kidato cha kwanza Butinzya sekondari Saieda Gusho alisema wanafunzi wengi
wanachelewa kutokana na wazazi wao kutowaanda watoto wao mapema kuwanunulia
vifaa vya shule hali ambayo inawafanya kupitwa na masomo ya awali.
Comments
Post a Comment