Zahanati ya Kijiji cha Ihulike katika muonekano wa hatua iliyofikiwa baada Mhe. Doto Biteko(Mb) kutoa mifuko 38 ya saruji ikiwa iliyotumika hadi sasa ni mifuko ya saruji 20 na kazi bado inaendelea
Katibu wa Umoja wa Wanawake wa CCM Wilaya ya Bukombe akizungumza na wakazi wa Ushirombo.
Huyu ni mmoja wa wenyeviti wa wakitongoji kupitia Chadema akikapidhi kadi ya chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Bukombe Daniel Machongo akipokea Mwanachama mpya kutoka Chadema
Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba akizungumza na wakazi wa Ushirombo.
Wananchi wa Kata ya Ushirombo Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita, wamepokea tathimini ya maendeleo ya kuanzia 2016 hadi 2018 iliyosomwa na Diwani wa Kata hiyo Lameck Warangi.
Akitoa tathimini hiyo Warangi alianza kwa kuishukuru serikali
na wadau wote wa Maendeleo kwa kuwashika mkono katika kuhakikisha Kata hiyo
inaendeleo kupata maendeo na kubainisha upande wa elimu kwa mafanikio makuwa
wanayoyapata kwa upande wa Sekondari ya Businda baada ya kuwa na maono ya kuwa
na kidato tano na sita katika shule hiyo.
Warangi alisema wanataraji ndani mwaka 2019 zahanati ya
Businda,Ihulike,Mwalo na Kiziba zitakuwa
zimeanza kutoa huduma kwa wananchi ili kupunguza adha ya kutembea umbali mrefu
kutafuta huduma ya afya.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bukombe said Nkumba
alimshukuru sana Mbunge wa Jimbo la Bukombe kwa namna ya pekee anavyojitoa
katika miradi ya maendeleo inayoendelea sehemu mbalimbali kwa Wilaya nzima na
kuwaomba wananchi wa Kijiji cha Ihulike kuongeza bidii zaidi ili kuunga mkono
jitihada za Mbunge wao baada ya kuwa ametoa mifuko 38 ya saruji kwa ajili ya
ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho.
Pia aliwasisitiza
wakazi wa Ushirombo na Wilaya nzima ya Bukombe kuhakikisha wazazi na walezi
wanawaandikisha watoto wao shule ili kumuunga mkono Raisi wa Jamhuri ya
Muungano Dkt John Pombe Magufuli kwa kutoa elimu bure sambamba na kusimamia kwa
kushirikiana na walimu ili kujua maendeleo ya watoto hao na kutengeneza taifa
la kesho lenye wasomi wengi.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Bukombe Daniel
Machongo aliwapongeza wakazi wa Ushirombo kwa kujitoa katika shughuli za
maendeleo bila kujali itikadi za vyama,dini wala ukabira na kuwakaribisha
viongozi waliohamia CCM kwa hiari yao kutoka chama pinzani cha Chadema ikiwa
katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2014 CCM walipoteza vitongoji vinane
kwa Kata ya Ushirombo na tayari wamesharudi wenyeviti wanne na wengine wakiwa
mbioni kujiunga na CCM.
Comments
Post a Comment