WAJASIRIAMALI WILAYANI BUKOMBE WAANZA KUGAWIWA VITAMBULISHO VYA RAIS MAGUFULI



 Meza Kuu  wakiwa tayari kwa uzinduzi wa ugawaji wa vitambulisho vya wajasiriamali wadogo uliofanyika katika Mji wa Ushirombo. 
 Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba akimkabidhi mmoja wa wajasiriamali wadogo wa Mji wa Ushirombo




WAJASIRIAMALI wadogo wadogo Wilaya ya Bukombe mkoani Geita  wameonywa kutotumia vitambulisho walivyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuuzia biashara za wafanyabiashara wakubwa na hivyo kuwa chanzo cha ukwepeji kodi.

Onyo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba wakati akizidua zoezi la ugawaji wa  vitambulisho kwa Wajasiriamali wa Mji wa Ushirombo.

Alisema vitambulisho vilivyotolewa na Rais ni kwa ajili ya Wajasiriamali wadogo wadogo na sio vinginevyo na ambao 
biashara zao kwa mwaka mapato yao hayazidi shilingi  milioni nne.


Said  alisema ni kosa kuazimisha kitambulisho au kubeba bidhaa za wafanyabiashara wakubwa  na kuongeza kuwa atakayebainika atakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Alisema wanaotakiwa ni wafanyabiashara wasio katika sekta isiyo kama vile mama na baba lishe na machinga na atatakiwa kulipia kitambulisho shilingi 20,000/baada ya kujaza fomu maalumu inayopatikana Ofisini kwake.

Comments