Waziri wa Madini na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akiwa na baadhi ya wafanyabiashara wakiangalia hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa choo cha soko la Kilimahewa(picha ni ya zamani).
Wafanyabiashara wa soko la Kilimahewa wakiwa katika umakini wa kumsikiliza Mhe. Doto Mashaka Biteko(Mb)
Tayari kwa Matumizi
Wafanyabiashara ndogo ndogo wa soko la Kilimahewa
lililopo Mji
wa Ushirombo Wilayani
Bukombe wamemshukuru Mbunge wa Jimbo la
Bukombe Mkoani Geita Mhe Doto Mashaka Biteko baada ya kuwashika mkono katika
ujenzi wa choo cha soko hilo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti sokoni hapo na Katibu wa soko la
wajasiliamali Kilimahewa Gaudesia Nzumbi alisema soko liliazishwa mwaka 2001 na
hadi sasa linameza 98 zinazofanyakazi na 80 wako nje ya soko pia kuna wenye
maduka na wafanyabiashara wa nguo wanao uzia chini.
Nzumbi alisema kabla
ya kujenga choo wafanyabiashara walikuwa wanajisaidia kwenye nyumba za majirani
na soko hilo na wengine vichakani hali ambayo ilikuwa changamoto kubwa kwa
wafanyabiashara hao.
Mkazi wa Kilimahewa Janeti Paul alisema wanaishukuru serikali na viongozi
wengine waliohamasisha au kushiriki katika ujenzi wa choo cha soko ili kulinda
Afya za wananchi wanaozunguka soko na wafanyabiashara wenyewe.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Katente Bahati Kayagila
aliwaomba wafanyabiashara hao kuendelea kuibua miradi ya maendeleo na kuchangia
maendeleo kila wanapo kubaliana kuanzisha mradi ili kupunguza au kuondoa
changamoto zinazo wakabili na serikali itawashika mkono.
Waziri wa Madini na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko aliwachangia
Tsh milioni 1.7 baada ya kuwatembelea na
kujionea hali halisi ya wafanyabiashara hao na kuona nia yao baada ya kuchangishana
wao kwa wao Tsh 4,000 kila mfanyabiashara kwa ajili ya ujenzi wa choo cha kisasa
ili waondokane na changamoto ya muda mrefu ya kujisaidia sehemu zisizokuwa
sahihi.
Comments
Post a Comment