Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt John Pombe Magufuli, leo amefanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri
na kuteua Mawaziri, Makatibu wakuu na Balozi,
Dkt. Mpoki Ulisubisya aliyekuwa Katibu
Mkuu Wizara ya Afya, ameteuliwa kuwa Balozi ambaye Ubalozi wake bado
haujatangazwa, na ndiye aliyeongoza timu ya madaktari kumuokoa Tundu
Lissu mkoani Dodoma.
Uteuzi huo ambao umetangazwa na Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, pia Rais Magufuli amemteua Bi. Angela
Kairuki kuwa Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu / Uwekezaji, na
kumpandisha cheo Naibu Waziri wa Madini Dotto Biteko kuwa Waziri wa
Madini, na Naibu wa pili wa wizara hiyo Stanslaus Nyongo kuendelea kuwa
Naibu Waziri.
Pia Rais Magufuli ameteua Makatibu Wakuu wanne, na Naibu Makatibu Wakuu wawili, ili kujaza nafasi za Makatibu Wakuu waliostaafu.
TAZAMA ORODHA KAMILI HAPA CHINI:
Angela Kairuki – Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu/Uwekezaji
Doto Biteko – Waziri wa Madini
Stanslaus Nyongo – Naibu Waziri Madini
Joseph Nyamhanga - Katibu Mkuu TAMISEMI
Zainabu Chaula – Katibu Mkuu Afya
Elius Mwakalinga – Katibu Mkuu Ujenzi
Doroth Mwaluko – Katibu Mkuu Sera
Doroth Gwajima - Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI
Francis K Michael - Naibu Katibu Mkuu UTUMISHI
Sambamba na hayo yote Rais Magufuli
amefungua Ubalozi mpya wa Tanzania nchini Cuba ambao utakuwa katika mji
wa Havana, na Balozi wake atatangazwa hivi karibuni.
Comments
Post a Comment