
Jeshi la Polisi mkoani Songwe limeeleza
sababu ya askari wa usalama barabarani kumshambulia dereva kwa kumpiga
kuwa alitumia lugha ya matusi na kutotii amri ya kumtaka atoe
ushirikiano kwa wanausalama hao ambao walikuwa wakifanya kazi kwa
kushirikiana na maofisa toka Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchikavu
(Sumatra).
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa
Yusuph Sarungi amewaambia waandishi wa habari leo Jumatatu Januari 14,
2019 kuwa tukio hilo lilitokea juzi Jumamosi Januari 12, 2019 saa 2:30
asubuhi katika eneo la Transforma, halmashauri ya mji wa Tunduma
wilayani Momba wakati askari hao wakishirikiana na maofisa toka Sumatra
wakiwa kwenye ukaguzi wa magari mbalimbali.
Amesema dereva huyo Mawazo Jairos (29)
mkazi wa Mbeya aliyekuwa akiendesha gari aina ya Mistubishi Fuso lenye
namba za usajili T842 AAC, baada ya kusimamishwa alianza kutoa lugha za
kashifa na matusi kwa askari na maofisa wa Sumatra.
Kamanda huyo amesema Jairos aliliondoa
gari bila ya kuruhusiwa kwa kupitia barabara ya vumbi hali iliyolazimu
askari hao kumfuatilia na kumkamata tena katika eneo la Makambini ambapo
walimzuia tena.
Sarungi amesema dereva huyo aliteremka kwenye gari kwa jazba huku akiendelea kutoa matusi na kumshambulia askari......
Na Stephano Simbeye, Mwananchi
Comments
Post a Comment