Jengo la Shule ya Sekondari Ushirombo linalotarajiwa kuezekwa
Makabidhiano ya Mabati
Benki ya NMB Tawi la Bukombe lakabidhi mabati 185 katika shule ya Sekondari Ushirombo na Compyuta saba kwa shule ya Sekondari Katente zilizoko Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita.
Wakati akikabidhi vifaa
hivyo Meneja wa Benki ya NMB Tawi la
Kahama Richard Kirengo kwa niaba ya Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi alisema changamoto za
sekta ya Elimu Tanzania kwa Benki ya NMB ni jambo la kipaumbele,kutokana na
ukweli kwamba Elimu ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa lolote hapa duniani.
“Tunatambua serikali inafanya
makubwa katika utoaji wa Elimu Bure na sisi kama wadau wa maendeleo tunawajibu
wa kuunga mkono juhudi hizi kwa
kuisaidia jamii”. Kirengo alisema
Nae Meneja wa Benki ya NMB Tawi
la Bukombe George Fundi alishukuru halmashauri na serikali ya wilaya ambavyo
imekuwa ikitowa ushirikiano NMB na kwamba wataendelea kushiriki katika miradi
ya maendeleo.
Kwa Upande wake Diwani wa Kata ya
Bulangwa Yusuph Mohamed amewaomba wananchi kuchangia miradi ya maendeleo kwa
hiari yao wanapoibua miradi na kuacha kuisubiri serikali iwafanyie kila
kitu.
Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said
Nkumba alitoa shukrani kwa Benki ya NMB kwa kuunga mkono jitihada za serikali
na kutoa wito kwa wadau wengine wa maendeleo kuendelea kutoa mali zao kwenye
miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa nguvu za wananchi na serikali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Dionis Myinga alisema atahakikisha maelekezo
ya Mkuu wa Wilaya yanafanyiwa kazi na kwamba wadau wa maendeleo waendelee
kuchangia miradi ya maendeleo.
Comments
Post a Comment