Tangu Mwalimu wa shule
ya msingi Nyahanga hadi kuwa Afisa Elimu Taaluma Wilaya ya Nyag’hwale na wadhifa wa umwenyekiti wa baraza la wazazi CCM Mkoa wa Geita, hatimae 2015 kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Bukombe na
kuteuliwa na Rais Dkt. John Magufuli kuwa Naibu Waziri wa Madini 2018 hadi Januari 8 mwaka 2019 kuteuliwa kuwa Waziri Madini na kuapishwa Januari 9 alipewa
dhamana ya kuendesha Wizara ya Madini kitu ambacho kilikuwa ni kiu ya muda
mrefu kwa wanabukombe kupata Waziri tangu Wilaya kuazishwa mwaka 1995.
Katika muonekano wa kawaida Mbunge wa Jimbo la Bukombe Doto
Biteko anaonekana anashirikiana na wananchi, viongozi wa serikali na chama
chake vizuri.
Tangu achanguliwe kuwa Mbunge Oktoba 25 mwaka
2015 amekua akijishugulisha na wananchi kupitia mikutano ya hadhara na wengine
kutumia njia nyingine kufanikisha maendeleo.
Kwa miaka mitatu aliyoiyafanya katika kuchagia maendeleo katika miradi iliyokuwa inaibuliwa na wananchi katika vitongoji 373 vijiji 52 kata 17 tarafa 3.
Kwa miaka mitatu aliyoiyafanya katika kuchagia maendeleo katika miradi iliyokuwa inaibuliwa na wananchi katika vitongoji 373 vijiji 52 kata 17 tarafa 3.
Biteko amesema feha za kuchochea shughuli za maendeleo kwa
kipindi cha mwaka 2015 hadi 2018 ametoa sh 102,037,797 zimetumika kutatua kero
za wananchi hasa sekta ya Elimu, Afya na Maji, na vikundi vya wajasiliamali na
kuchangia ujenzi wa vituo vidogo vitatu
vya polisi.
Amesema Jimbo la Bukombe linaukubwa wa kilometa za mraba
zipatazo 8,055.59 kati yahizo kilometa za mraba 1766.59 ambazo sawa na asilimia
21.93 eneo la makazi na eneo linalo baki kilomita 6289 ni eneo la hifadhi za
TFS na pori la hakiba Kigosi Muyowos huku jimbo lina watu 224,542 kutokana na
sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012.
Biteko amesema kutokana na ziara ambazo amekuwa akizifanya
katika kipindi cha mwaka 2015 hadi Desemba 2018 ameulizwa na wananchi maswali
2567 ambayo yameulizwa kata zote 17 kutokana na kero mbali mbali zilizokuwa
kwenye huduma za kijamii.
Kero hizo nilizikabiri kwa kushirikiana na madiwani na
watalamu wa halmashauri na wadau wa maendeleo zipo changamoto ambazo zimetatuliwa
kwa haraka na nyingine ninaendelea kuzitatua awamu kwa awamu na mabadiliko
yanaonekana.
Amesema wakati anachaguliwa 2015 kulikuwa na zahanati nne
vituo vya Afya viwili, lakini kwa sasa Jimbo la Bukombe lina zahanati 10 vituo
vya Afya vinne na kwa kipindi cha mwaka 2018 katika kuhakikisha serikali
inasongeza huduma kwa wananchi tumepata fedha kwa ajili ya upanuzi wa kituo cha
Afya Uyovu na Ushirombo.
Mwaka 2015 kulikuwa na mtandao wa barabara kilomita 256,
lakini mpaka 2018 mtandao wa barabara umeongezeka kufikia zaidi ya kilomita 1500 na kuwa Wilaya ya pili
kimkoa kuwa na mtandao mkubwa wa barabara.
Amesema kuwa kutokana na serikali kuongeza bajeti ya wakala
wa usambazaji wa umeme vijiji (REA) nimeendelea kufuatilia na kuhakikisha
umeme unasabazwa vijiji vyote vya Wilaya ya Bukombe ili kufikia
malengo ya kuifanya Bukombe nzima ipate Umeme na nguzo zinaendelea kusambazwa
na mkandarasi.Biteko amesema.
Mkazi wa kijiji cha Uyovu Ester Maganga amsema kuwa maendeleo
ya tofauti wameyaona tofauti na miaka mingine
wamekuwa wakiona maendeleo bila kuchangishwa wananchi ikiwemo shule ya
watoto wenye mahitaji malumu iliyopo shule ya msingi Uyovu na Ushirombo.
Maganga ameongeza kuwa Mbunge ni wakati wa kujitathimini
kupitia aliyoyafanya kwa miaka mitatu na kwamba asije akachoka kuwaletea
maendeleo wana Bukombe ili uchanguzi mkuu 2020 atumie dakika 45 na za nyogeza 3
ili kuwa na historia ya kwenda Bungeni
awamu mbili na huenda Rais Magufuli ataendelea kumuacha na nafasi yake.
Katibu mkuu wa CCM Taifa
Bashiru Ally amesema wakati wa ziara
yake Wilaya ya Bukombe wakati Mbunge Biteko anawasilisha taarifa ya utekelezaji
wa Ilani ya CCM kwa aliyoyafanya kwa
miaka mitatu alimpongeza.
Ally aliwahimiza wabunge na viongozi wa chama na serikali
kusimamia sekta ya kilimo ikiwa ni nguzo inayotegemewa na taifa kwa kuinua
uchumi kwa wananchi wake hivyo wasaidizi
wa Rais Dk John Magufuli kuanzia ngazi ya Wilaya na Mkoa kushuka chini
wahakikishe wanaelimisha wakulima namna ya matumzi ya mbegu bora
Ally aliwataka Wakuu wa Wilaya na Mkoa kuhamasisha wakulima
kulima na kupanda mbegu bora na kufunga mifungo kwa kuzingatia ufungaji wa
kitalamu ili kupata maligafi kwenye viwanda wakati Tanzania ikielekea kwenye
uchumi wakati na viwanda.
Mkuu wa Wilaya ya
Bukombe Said Nkumba amewaomba wananchi wilayani hapa kuunga mkono jitihada za
wadau wa maendelo ili kufikia malengo ya miradi walio ianzisha.
Nkumba amesema Mbunge kwa namna ya pekee anavyojitoa katika
miradi ya maendeleo inayoendelea sehemu mbalimbali wilayani hapa sekta ya Elim
na Afya wananchi na wadau wa maendeleo inawapasa kumuunga mukono.
Comments
Post a Comment