Michezo ya kubatisha nchini Tanzania
imekuwa maarufu huku washiriki zaidi wakiwa vijana lakini sasa Bodi ya
Michezo ya Kubahatisha imezuia kwa muda urushaji wa matangazo ya michezo
hiyo kupitia redio na televisheni.
Bodi hiyo imedai kuwa matangazo hayo yamekuwa mengi kiasi cha kuharibu taswira ya mchezo huo.
Taarifa ya bodi hiyo ya Januari 23, 2019
iliyosainiwa na kaimu mkurugenzi mkuu, James Mbalwe inaeleza kuwa hatua
ya kusitisha matangazo hayo ni kutokana na malalamiko miongoni mwa
wananchi juu ya kukithiri kwa matangazo kwenye vyombo hivyo vya habari.
“Kumekuwa na ongezeko la malalamiko
kutoka kwa umma juu ya kukithiri kwa matangazo ya michezo ya kubahatisha
hapa nchini,” inaeleza taarifa hiyo.
“Bodi imesitisha kwa muda urushaji wa
matangazo ya michezo ya kubahatisha kupitia redio na televisheni.
Matangazo yanayotolewa kupitia vyombo vingine hayaathiriwi na zuio
hili.”
Comments
Post a Comment