
Mkazi wa kitongoji cha Mwibale wilayani
Serengeti, Chibona Matoyo (64) akihojiwa na Mwandishi wa gazeti la
Mwananchi, Daniel Makaka (kushoto) baada ya bibi huyo kunusurika kifo
kufuatia kushambuliwa na mamba alipokuwa akioga ndani ya Ziwa Victoria,
wilayani humo.
Chibona Matoyo (64), mkazi wa Kijiji
cha Kanyala Wilaya ya Sengerema, Mara amenusurika kifo baada ya
kujeruhiwa na mamba wakati akioga katika Ziwa Victoria.
Katika tukio hilo lilitokea Alhamisi
iliyopita, Chibona alivunjika mikono na kujeruhiwa paji la uso na sasa
anapatiwa matibabu kwenye Kituo cha Afya Mwangika, Buchosa wilayani
humo.
Akizungumza na Mwananchi jana, mama huyo
mwenye watoto watano na wajukuu tisa, alisema wavuvi ndio waliookoa
maisha yake baada ya kupiga kelele akiomba msaada.
“Walipoona napiga kelele walifika eneo la tukio na kunikuta napambana na mamba, walinisaidia kujinasua, walifanikiwa,” alisema.
Baada ya kupata taarifa za tukio hilo,
mume wa Chibona, Ernest Majula (81) aliangua kilioakisema mkewe amepata
kilema na kuiomba Serikali kuchukua hatua kuwadhibiti wanyama hao.
Mtoto wa mama huyo, Agnes Majula alisema
wamekuwa na mazoea ya kwenda kuoga ziwani wakiamini kuwa kufanya hivyo
ni vizuri zaidi kuliko majumbani mwao.
Daniel Makaka - Mwananchi
Comments
Post a Comment