Basi la shule ya msingi Little Treasures
iliyopo katika manispaa ya Shinyanga imepata ajali na kupinduka na
kutumbukia mtaroni eneo la Kalogo mjini Shinyanga na kusababisha
majeraha kwa wanafunzi kadhaa.
Ajali hiyo imetokea leo Alhamis Januari
10,2019 majira ya saa tisa alasiri wakati basi hilo lenye namba za
usajili T183 AFE likitoka shuleni eneo la Bugayambelele kata ya Kizumbi
kuelekea Ushirika likirudisha wanafunzi majumbani.
Akizungumza na Malunde1 blog, Kamanda wa
polisi mkoa wa Shinyanga, ACP Simon Haule amesema hakuna madhara
makubwa yaliyotokea bali baadhi ya wanafunzi wamepata majeraha madogo
madogo.
Amesema basi hilo lilikuwa limebeba
wanafunzi 30 na tayari waliojeruhiwa wamepatiwa matibabu kati yao wanne
bado wapo hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
"Basi lilikuwa linatoka shuleni
likipeleka wanafunzi/watoto majumbani mwao,lilipofika eneo la Kalogo
karibu na ofisi za TANROADS likapinduka na kusababisha majeraha kwa
wanafunzi ambao wamekimbizwa katika hospitali ya rufaa mkoa wa Shinyanga
ambapo baadhi wamepatiwa matibabu na kuruhusiwa kutoka ,wanne bado
wanapatiwa matibabu",amesema Kamanda Haule .
Kamanda Haule amekitaja chanzo cha ajali
hiyo kuwa ni dereva wa gari hilo kuendesha huku akichezea simu/akichat
na baada ya ajali kutokea alikimbia na wanaendelea kumtafuta.
Muonekano wa gari la shule ya Little Treasures baada ya kupata ajali - Picha na Steve Kanyefu - Malunde1 blog
Comments
Post a Comment