WANANCHI WAHAMASISHWA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI ILI KUDHIBITI UHALIFU

 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Bashiru Ally akipokea zawadi ya asali mbichi kutoka kwa wazee Maarufu wa CCM Wilaya ya Bukombe.



 Mbunge wa Jimbo la Bukombe na Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Ilani tangu 2015 hadi 2018 kwa njia ya kidigitali (Projector) kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Wilaya Bukombe.

 
 Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Wilaya Bukombe wakiwa kwenye kikao cha kusikiliza taarifa ya Utekelezaji wa Ilani tangu 2015 hadi 2018 ikisomwa na Mbunge wa Jimbo la Bukombe na Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko.


  Katibu Mkuu wa CCM Taifa Bashiru Ally akimpa mkono wa pongezi Mhe Doto Mashaka Biteko(Mb) baada ya kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Ilani tangu 2015 hadi 2018 kwa njia ya kidigitali (Projector) kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Wilaya Bukombe.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya Bukombe Daniel Machongo akimpa mkono wa pongezi Mhe Doto Mashaka Biteko(Mb) baada ya kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Ilani tangu 2015 hadi 2018 baada ya kupokelewa na wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Wilaya Bukombe.







 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Bashiru Ally akimkabidhi Pikipiki na kadi zake tatu   Mkuu wa Polisi Wilaya Bukombe(OCD) Thedius Kaihuzi







Wananchi wa Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita, wametakiwa kutoa ushirikiano kwenye jeshi la Polisi wakati wa upelelezi wa kuwasaka wahalifu ili jeshi hilo liweze kufanyakazi zake kwa urahisi.

Wito huo ulitolewa na Katibu Mkuu wa Ccm Taifa Bashiru Ally wakati akikabidhi piki piki tatu zenye thamani ya sh milioni  7.3 kwa Mkuu wa  Polisi Wilaya ya Bukombe kwa ufadhili wa Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko  ambazo zitasambazwa kwenye vituo vidogo vya polisi kwa ajili ya kupambana na uhalifu.

Ally alisema nchini hapa polisi niwachache na wanakabiliwa na changamoto ya upungufu wa usafiri na  wamekuwa wakifanya vizuri ingawa wanakabiliwa na changamoto hizo hali  ambayo imekuwa  ikileta tija kwa wananchi.

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka  Biteko awali akitoa Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Ccm kwenye Mkutano Mkuu wa Wilaya ya Bukombe katika kipindi cha miaka mitatu 2015 hadi 2018 alisema tangu mwaka huo kulikuwa na vituo vya polisi viwili, kituo kikubwa cha Wilaya na kidogo cha Runzewe.

Biteko alisema kutokana na hali hiyo kulikuwa na uhalifu wa ujambazi kuvamia wafanya biashara wizi wa ng,ombe na likaibuka wimbi la kutekwa watoto wa wafugaji na polisi walipambana na kufanikisha kudhibiti uhalifu huo hadi sasa Bukombe nishwari.

Alisema kutokana na serikali kusongeza huduma kwa wananchi wamefanikisha kusongeza huduma ya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na wananchi .kujenga vituo vitatu vidogo vya polisi  kwa lengo kubwa  la kudhibiti uhalifu na nimetoa pikipiki  ili ziwalahisishie polisi kwenye vituo vipya utendaji kazi.

Mkuu wa polisi wilaya ya Bukombe Thedius Kaihuzi alishukru msaada huo nakuongeza kuwa piki piki watazitunza na zitawasaidia kufika kwenye tukio kwa wakati askari ili kupambana na uhalifu nakwamba piki piki hizo zitapelekwa kwenye kituo cha pilisi Namonge , Bukombe na Bulenga.



Comments