Vifo
vilivyo sababishwa na ugaidi vimepungua katika kipindi cha miaka mitatu
iliyopita duniani, tafiti mpya iliyohusisha nchi zote duniani
imegundua.
Tafiti
ya sita ya kila mwaka juu ya hali ya ugaidi duniani, iliochapishwa na
Taasisi yenye kuangalia hali ya uchumi na amani yenye ofisi zake Sydney
(IEP), imesema vifo vinavyotokana na ugaidi vimepunguwa duniani kwa
asilimia 27 mwaka 2017, ikiwa ni mwaka wa tatu mfululizo idadi ya vifo
hivyo kupungua.
Hata hivyo, ugaidi umebaki kuwa ni tishio kubwa kwa usalama wa dunia, ripoti hiyo imeeleza.
Ripoti hiyo inaonyesha kuwa mashambulizi ya kigaidi mengi yanaziathiri nchi ambazo zinavurugu nyingi za kisiasa.
Nchi
kumi ambazo zimeathiriwa zaidi na ugaidi ni Afghanistan, Iraq, Nigeria,
Somalia, Syria, Pakistan, Misri, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,
Jamhuri ya Afrika ya Kati na India.
“Migogoro na ugaidi wa kitaifa ni njia kuu za kusababisha ugaidi,” ameandika Steve Killelea, mwenyekiti mtendaji wa IEP.
Maeneo
yaliyo hatarishi katika ugaidi “yote yalihusika kwa angalau mgogoro
mmoja wenye uvunjifu wa amani, na nane yaliingia katika vita kubwa na
kusababisha vifo sio chini ya 1,000. Hizi nchi 10 zilichangia asilimia
84 ya vifo vilivyotokana na ugaidi mwaka 2017,” repoti hiyo imeeleza.
Chanzo:Voa
Comments
Post a Comment