SERIKALI YAFUTA MITIHANI YA KIDATO CHA PILI

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imefuta mitihani ya kidato cha pili visiwano humo iliyokuwa ikiendelea na kusema kuwa tarehe ya mitihani hiyo itatangazwa tena.

Akizungumza na wanahabari leo Disemba 3, 2018, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Aamali Zanzibar, Riziki Pembe amesema kuwa mitihani hiyo ifutwe na wanafunzi waendelee na masomo yao kama kawaida.

"Wizara imefuta mitihani hiyo na itatangaza tena tarehe ya kurudiwa, mara tu taratibu zitakapo kamilika", amesema Bi. Pembe.

Mitihani hiyo imeahirishwa ikiwa ni muda mfupi tangu kwa upande wa Tanzania bara, kukamilisha mitihani hiyo Novemba 24,2018.
Chanzo - EATV

Comments