Kocha Jose Mourinho amefutwa kazi na Manchester United ikiwa ni siku moja tu imepita tangu afungwe mabao 3-1 na Liverpool.
Kupitia
taarifa yake leo, Man United imeeleza kuwa imefikia uamzi huo ili
kunusuru mwenendo wa klabu katika michuano mbalimbali inayoshiriki
ikiwemo EPL na klabu bingwa Ulaya.
"Klabu
inamshukuru Jose kwa kazi yake nzuri wakati akiwa na Manchester United
na tunamtakia mafanikio katika kazi yake hapo baadaye'', imeeleza
taarifa ya klabu.
Kiungo
wa zamani wa timu hiyo Michael Carrick ametangazwa kuchukua nafasi ya
Jose Mourinho kama kocha wa muda wa Manchester United mpaka mwisho wa
msimu huu wa 2018/19.
Mourinho
alijiunga na Manchester United Juni 2016 akiwa kocha huru baada ya
kufukuzwa na Chelsea. Amedumu na Man United kwa takribani miaka miwili
na nusu.
Comments
Post a Comment