
Mwili
wake ulisafirishwa kwa treni maalumu hadi mji wa College Station huko
Texas na alizikwa kwenye eneo la chuo kikuu cha Texas A&M
Wakazi
wa jimbo la Texas nchini Marekani walimuaga Rais wa 41 wa Marekani,
George Herbert Walker Bush siku ya Alhamis kabla ya mwili wake
kusafirishwa kwa treni maalumu kuelekea sehemu ya mapumziko yake ya
mwisho.
Treni
ilianza safari kuelekea mji wa College Station mahala alipozikwa kwenye
eneo la chuo kikuu cha Texas A&M. Mara baada ya treni kuwasili
ilipokelewa na bendi ya jeshi. Pia jeshi la majini la Marekani lilirusha
ndege 21 za vita angani na kutoa saluti kwa nahodha wa majini wa vita
ya pili ya dunia ikifuatiwa na ufyatuaji mizinga 21.
George
H.W. Bush alizikwa pembeni ya kaburi la mke wake Barbara Bush
waliyeishi nae kwa miaka 73. Barbara alifariki mwanzoni mwa mwaka huu.
Hii
Ilikuwa mara ya kwanza treni kuubeba mwili wa Rais kwa mazishi tangu
mwili wa Dwight D. Eisenhower aliyekuwa Rais wa 34 wa Marekani
ulipobebwa na treni kutoka Washington DC kwenda kwenye jimbo lake la
Kansas nchini Marekani miaka 49 iliyopita.
Chanzo:Voa
Comments
Post a Comment