
Makao Makuu madogo ya CCM Dar es salaam.
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kasulu
Mjini ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu, Moses Machali,
amesita kuzungumzia safari yake ya kuelekea kwenye uchaguzi Mkuu wa
mwaka 2020 na kubainisha kuwa hajui kama atawania nafasi yeyote.
Machali amesema hawezi kuzungumzia
nafasi ya kurudi bungeni kwa sasa kutokana na kubanwa na taratibu za
chama chake ambazo zinamkataza mwananchama wa kawaida kuonesha nia ya
kuwania nafasi yeyote wakati kuna viongozi husika.
"Kuhusu suala la kugombea tena ubunge
kupitia CCM kwa sasa sina cha kusema, sitaongea kwa sasa kwa sababu
nitakuwa nimekiuka misingi ya chama, kwa hiyo nahifadhi maneno yangu," amesema Machali.
"Hata uniulize kwa namna gani,
msimamo wangu kugombea nafasi yeyote 2020 bado nitaendelea kutosema
chochote, mpaka wakati muafaka utakapowadia" ,ameongeza Machali.
Moses Machali aliteuliwa na Rais
Magufuli, Julai 28 mwaka huu kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu pamoja na
makada wengine waliohama kutoka upinzani na kujiunga na CCM, akiwemo
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini, Patrobas Katambi na David Kafulila
ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe.
Chanzo-EATV
Comments
Post a Comment