Meenakshi Valand ni mwananamke wa 12 duniani kujifungua mtoto baada ya kupandikizwa mfuko wa uzazi
Meenakshi Valand ni mmoja kati ya watu wachache duniani ambao wamejaaliwa kupata watoto baada ya kupandikizwa mfuko wa uzazi.
"Sikuweza
kujizuia kulia baada ya kusikia sauti ya mwanangu akilia. Haya ni
machozi ya furaha - Nimepoteza watoto sita katika kipindi cha miaka
kadhaa iliyopita," alisema Meenakshi.
Mama huyo wa miaka 28-alijifungua mwezi uliyopita nchini India baada ya kupandikizwa mfuko wa uzazi wa mamake mzazi.
Katika
miaka tisa ya ndoa yake, Meenakshi alizaa watoto wawili waliofariki,
alipoteza wengine wanne katika uja uzito, hatua iliyomsababisha kukatika
kwa mfuko wake wa uzazi.
Chanzo:Bbc
Comments
Post a Comment