
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania
linasikitika kutangaza kifo cha Askofu Evaristo Marcus Chengula wa Jimbo
Katoliki la Mbeya kilichotokea, Jumatano, tarehe 21 Novemba 2018 majira
ya saa 3:00 asubuhi kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Jijini Dar
es Salaam.
Akizungumza na Vatican News, Padre Charles Kitima, Katibu mkuu wa Baraza
la Maaskofu Katoliki Tanzania amesema, Marehemu Askofu Chengula
aliwasili Jijini Dar es Salaam, Jumanne, tarehe 20 Novemba 2018 akiwa
anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo.
Akapelekwa na kulazwa Muhimbili, jitihada za Madaktari kutaka kuokoa
maisha yake, zikagonga mwamba na Askofu Evaristo Marcus Chengula akaaga
dunia katika usingizi wa amani, akiwa na tumaini la ufufuko na maisha ya
uzima wa milele!
Askofu Evaristo Marcus Chengula alizaliwa tarehe Mosi Januari 1941, huko Mdabulo, Wilaya y Mufindi, Mkoani Iringa.
Baada ya masomo na majiundo yake ya kitawa na kipadre, tarehe 15 Oktoba 1970 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre.
Tarehe 8 Novemba 1996, Mtakatifu Yohane Paulo II akamteua kuwa Askofu wa
Jimbo Katoliki Mbeya na kuwekwa wakfu kama Askofu tarehe 2 Februari
1997.
Amefariki dunia akiwa amelitumikia Kanisa kama Padre kwa muda wa miaka 48 na Askofu kwa muda wa miaka 21!
Apumzike katika usingizi wa amani, akiwa tayari kukutana uso kwa uso na Kristo Yesu, Hakimu mwenye huruma na mapendo!
Chanzo - Vatican News
Apumzike katika usingizi wa amani, akiwa tayari kukutana uso kwa uso na Kristo Yesu, Hakimu mwenye huruma na mapendo!
Chanzo - Vatican News
Comments
Post a Comment