
Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini
Tanzania (Tanzania Food & Drugs Authority – TFDA) imeendesha mafunzo
kwa Wasindikaji wadogo wa chakula mkoa wa Shinyanga ili kuwa
wezesha kujua sheria,kanuni na miongozo inayohusu usindikaji wa chakula salama pamoja na kuongeza kiwango cha uzingatiaji wa kanuni bora za uzalishaji chakula.
wezesha kujua sheria,kanuni na miongozo inayohusu usindikaji wa chakula salama pamoja na kuongeza kiwango cha uzingatiaji wa kanuni bora za uzalishaji chakula.
Mafunzo hayo ya siku mbili yaliyoanza leo Alhamis Novemba 22,2018
yanayofanyika katika ukumbi wa SIDO mjini Shinyanga, yamefunguliwa na
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa
Shinyanga,Zainab Telack.
Akifungua mafunzo hayo,Mboneko alisema mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa
mikoa inayokabiliwa na changamoto kubwa ya wajasiriamali na
wafanyabiashara kutokidhi matakwa ya kisheria yanayosimamiwa na
TFDA,TBS na TRA.
“Wafanyabiashara wakubwa na wadogo wamekuwa wakikiuka sheria kwa
kuweka vyakula na vinywaji nje ya maduka,vyakula vinapigwa na jua kila
siku halafu bidhaa hizo zinatumiwa na wananchi,hii inahatarisha afya za
walaji”,alisema Mboneko.
“Natoa rai kwa uongozi wa TFDA kuendelea kushirikiana na
wajasiriamali na wafanyabiashara waaminifu ili wawape taarifa za
wajasiriamali na wafanyabiashara wasio waaminifu na kuwachukulia hatua
kali za kisheria”,aliongeza Mboneko.
Kwa upande wake,Kaimu Mkurugenzi wa TFDA,Justin Makisi alisema kutokana
na kuwa suala la usafi ni changamoto kubwa inayovikabili viwanda vidogo
nchini,mafunzo hayo yatawezesha wasindikaji hao wadogo wa vyakula
kujifunza kanuni za usafi ili kutambua mambo ya msingi wanayopaswa
kuzingatia kitaalamu.
“Ili kuhakikisha vyakula vinavyosindikwa vinakuwa salama na bora kwa
ajili ya kulinda afya za walaji,TFDA imeamua kutoa mafunzo kwa
wasindikaji wadogo wa vyakula ambao ukweli ni kwamba bidhaa zao
zinasambaa sana, ili kuwapa mbinu za kuwasaidia bidhaa zao zimudu
ushindani wa soko na ndani na nje ya nchi”,alisema.
“Tayari tumetoa mafunzo kama haya kwenye mikoa 23,mkoa wa Shinyanga ni
wa 24,tunatoa mafunzo haya kwa kushirikiana na TBS na SIDO ikiwa ni
sehemu ya utekelezaji kwa vitendo azma ya serikali ya awamu ya tano
inayoongozwa na Mheshimiwa Rais,Dkt.John Pombe Magufuli ya kuwa na
uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda ifikapo 2025”,alieleza Makisi.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akifungua mafunzo kwa
Wasindikaji wadogo wa chakula mkoa wa Shinyanga kwa niaba ya mkuu wa
mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack leo katika ukumbi wa SIDO mkoa wa
Shinyanga - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza wakati akifungua
mafunzo kwa Wasindikaji wadogo wa chakula mkoa wa Shinyanga.Kulia ni
Mkaguzi Mkuu wa Chakula TFDA,Lazaro Mwambole.Kushoto ni Mwenyekiti wa
mafunzo hayo,Juma Nyankanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza na wasindikaji wadogo wa chakula mkoa wa Shinyanga.
Wasindikaji wadogo wa chakula mkoa wa Shinyanga wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko.
Kaimu Mkurugenzi wa TFDA,Justin Makisi akielezea lengo la Mamlaka ya
Chakula na Dawa nchini Tanzania kuendesha mafunzo kwa wasindikaji wadogo
wa chakula ili kuwawezesha kujua sheria,kanuni na miongozo inayohusu
usindikaji wa chakula salama pamoja na kuongeza kiwango cha uzingatiaji
wa kanuni bora za uzalishaji chakula.Kulia ni Meneja wa TFDA Kanda ya
ziwa Moses Mbambe,kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta
Mboneko.
Kaimu Mkurugenzi wa TFDA,Justin Makisi akiwataka wasindikaji wadogo wa
chakula kufuata sheria,kanuni na miongozo inayohusu usindikaji wa
chakula salama.
Kaimu Mkurugenzi wa TFDA,Justin Makisi akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Afisa Mkuu Mawasiliano na Elimu kwa umma TFDA Makao Makuu, James Ndege
akitaja mada zitakazofundishwa kwa wajasiriamali/wasindikaji wa chakula
ambazo ni dhana ya usalama wa chakula,taratibu za kisheria za usajili wa
majengo ya kusindika chakula na kutoa vibali vya kusindika
chakula,taratibu za kisheria za usajili wa vyakula
vilivyofungashwa,ufungaji na vifungashio,uwekaji lebo kwenye
vifungashio,teknolojia ya kusindika chakula,taratibu za utoaji alama ya
ubora n.k.
Wasindikaji wadogo wa chakula mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.
Awali Mkaguzi Mkuu wa Chakula TFDA,Lazaro Mwambole akimtambulisha,Meneja
wa TFDA Kanda ya ziwa Moses Mbambe (wa pili kulia) na Kaimu Mkurugenzi
wa TFDA,Justin Makisi (wa tatu kutoka kushoto).
Mkaguzi Mkuu wa Chakula TFDA,Lazaro Mwambole akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo wakiwa ukumbini.
Wawezeshaji wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini.
Picha ya pamoja,Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta
Mboneko,maafisa wa TFDA na wasindikaji wadogo wa chakula mkoa wa
Shinyanga kundi la kwanza.
Picha ya pamoja,Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta
Mboneko,maafisa wa TFDA na wasindikaji wadogo wa chakula mkoa wa
Shinyanga kundi la pili.
Comments
Post a Comment