Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),
ambaye pia ni Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, anatarajiwa kuagwa rasmi
kesho chuoni hapo baada ya kumaliza kipindi chake.
Rais Mkapa amekuwa mkuu wa chuo hicho tangu kianze mwaka 2007 hadi sasa.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo hicho
(Taaluma), Prof. Peter Msoffe, akizungumza na waandishi wa habari,
alisema ataagwa kwenye mahafali ya tisa yanayotarajiwa kufanyika Novemba
kesho chuoni hapo.
Alisema kwa mujibu wa hati idhini ya
chuo, Mkapa anatarajiwa kumaliza muda wake Machi 2019 na kwamba kwa kuwa
ni mahafali yake ya mwisho, wameamua kumuaga kesho.
Alisema Mkapa ameshakitumikia chuo kwa kipindi cha miaka 11 zikiwa ni awamu mbili tangu kuanzishwa kwake.
Alisema UDOM itaendelea kuvuna busara zake hata baada ya kumaliza na amekuwa nguzo imara ya chuo hicho.
Aidha, Prof. Msoffe alisema katika mahafali hiyo ya tisa ya mwaka huu kutakuwa na jumla ya wahitimu 7,122 kwa ngazi mbalimbali.
Alisema mahafali hiyo itatanguliwa na
kongamano la tisa la chuo hicho litakalofanyika leo na litakaloongozwa
na Balozi wa India nchini, Sandeep Arya, ambaye atawasilisha mada juu ya
maisha ya mwanzilishi wa Taifa la India, Mahatma Gandhi na mchango wake
katika jamii.
Comments
Post a Comment