BARAZA MAALUM LA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUKOMBE MKOANI GEITA YAJADILI MAPENDEKEZO YA KUMEGA ENEO KUTOKA KWENYE MAPORI YA AKIBA

Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita Denis Bandisa(Katikati),Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba(kulia), Katibu wa Umoja wa Vijana CCM Wilaya ya Bukombe Wambele Ngemela(wa pili kulia), Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Mhe. Lameck Warangi(kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Dionis Myinga kwa pamoja wakiwa meza kuu.

Wajumbe ambao ni madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Bukombe wakifuatilia  taarifa na maadhimio juu ya kikao ambacho kinaendelea.

Mkuu  wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba akizungumza na wajumbe wa Baraza la Madiwani wa Wilaya ya Bukombe.


Mkuu wa Kanda Kikosi cha kupambana dhidi ya ujangiri  Kanda ya Ziwa James Karomba akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa Baraza la Madiwani wa Wilaya ya Bukombe juu ya umuhimu wa uhifadhi na faida zake.

Diwani wa Kata ya Runzewe Mashariki Mhe. Maduhu Mwanambati akizungumza na wajumbe wa Baraza la Madiwani wa Wilaya ya Bukombe juu ya mapendekezo  ya kupata maeneo ya marisho ya mifugo kwa kumegewa kutoka kwenye mapori ya hifadhi.
.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita Denis Bandisa  akizungumza na wajumbe wa Baraza la Madiwani wa Wilaya ya Bukombe "tusiyaharibu mapori ya  hifadhi  kwa kuvunja sheria ya kuingia  ndani ya hifadhi hizo na kufanya shughuli za kibinadamu  kinyume cha sheria ni kosa nawasihi kutii sheria bila shuruti ili kuepuka migogoro isiyokuwa ya lazma" alisema Denis.

Muonekano wa Wajumbe wa Baraza la Madiwani wa Wilaya ya Bukombe lililofanyika leo katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe.

Comments